Kuna zile nguo tunanunua kwenye mitumba, dukani zikiwa zime chakaa au zipo nyumbani zime chakaa na bado tuna penda kuendelea kuzivaa. Hizi ni namna 10 una weza kubadilisha muonekano wa kuchakaa na kupata muonekano mpya kabisa
1)Badilisha Vifungo
Kubadilisha vifungo kutoka vile vya zamani kwenda vipya na vyenye style mpya vitabadilisha na kuinua muonekano wa vazi lako mara moja kama ni koti, sketi, shirt etc, hakikisha vifungo vinaendana rangi na vazi lako
2) Peleka nguo zako dry cleaner
Kwa sasa hawa wale wauza mitumba kabla ya kuanza kuuza nguo zao wana peleka dry cleaner zika fuliwe na kukaushwa uta shangaa jinsi ambavyo utazifuata zikiwa updated tofauti na ulivyo zipeleka
3) Ondoa urembo usio kuwa na lazima
Kuondoa urembo ambao hauhitajiki usio na lazima utaupa kama ni mkoba au vazi lako muonekano mpya.
4) Jali vitu vyako
tumia muda kujali vitu vyako kama viatu, mikoba,nguo hii itafanya hata kama nguo zako si za bei ghali, eg futa pochi la leather na mafuta ili kuondoa mikwaruzo, tumia tissue paper kuifadhi bags zako kabla ya kuziweka mahali
5) Nunua mavazi ya kiume
mara nyingi mavazi ya kiume huwa yana vitambaa bora zaidi, nunua size ndogo ambayo ina weza kukutosha vitu kama shirts, sweta au koti.
6) Tembelea Kwa Fundi Viatu
once in a while peleka viatu vyako kwa fundi viatu aka vifanyie usafi, au kubadilisha soli na kukipa kiatu chako muonekano mpya
7) Hifadhi vitu vyako vizuri
Hifadhi vitu vyako vizuri kama nguo chafu weka katika dustbin usitupe tupe hovyo na zilizo safi kunja au ning’iniza katika hanger hii itasaidia kufanya nguo zako kuwa na muonekano mzuri kila siku na kuto kupoteza upya wake
8)Peleka nguo kwa fundi nguo
Badilisha muonekano wa nguo mfano koti lenye mikono mirefu fanya liwe na mikono mifupi, bana suruali pana, badilisha suruali kuwa pensi. Jaribu vitu vipya kila siku uta pata mionekano mipya kila siku
9)Badilisha mikanda ya bag
9
katika ma begi kitu cha kwanza kuchakaa ni mikanda na vile vyuma kuchakaa, kama the rest of the bag bado ina dai (kuonekana mpya) unacho takiwa kufanya ni kwenda kwa fundi viatu au fundi yoyote anaye weza kubadilisha hizo chuma na mikanda, ili kupata muonekano mpya & expensive
Related posts
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…