SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Njia 6 Rahisi Za kupunguza Uzito Bila Ya Kutumia Diet
Dondoo

Njia 6 Rahisi Za kupunguza Uzito Bila Ya Kutumia Diet 

Wakati wengi wamemaliza kufunga Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kupungua uzito wengi watakuwa wanajiuliza namna ambavyo wanaweza ku-maintain mwili wako ubaki hivyo hivyo bila ya kuongezeka huku wengine wakiwa wanateseka na namna wanaweza kupunguza miili yao bila ya kufanya mazoezi na kufanya diet kali.

Kuna njia rahisi kama unaweza kujizoesha kufanya basi unaweza kupunguza uzito lakini pia kuwa na afya kipindi chote, hizi tumetoa katika life style ya wa China, China inasifika kwa kuwa watu wake wana afya nzuri unaweza kukutana na mzee ana tembea ana fanya mazoezi yupo fit lakini hii inatokana na jinsi wanavyo chagua kula na kuishi.

 • Maji Mengi

Washauri wengi wa mambo ya afya wanashauri kunywa maji lita zaidi ya mbili kwa siku kama ungependa kuwa na afya nzuri lakini pia husaidia kupunguza uzito, unapo kunywa maji mara kwa mara kunakufanya uhisi shibe na kukufanya kuto kutaka kula kula au kutafuna tafuna mara kwa mara.

 • Green Tea

Wachina wamekuwa wakiwa wamezingatia kunywa chai ya kijani kwa miaka mingi. Wanaamini kwa uwezo wake wa kusafisha mwili kutokana na  sumu yoyote kwakuwa inaaminika kuwa na  antioxidant nyingi. Zaidi ya hayo, kunywa kikombe cha chai ya kijani baada au wakati wa mlo husaidia kuondokana na tamaa ya kunywa vinywaji vingine visivyo na afya kama soda au mvinyo

NAMNA 5 ZA KUPUNGUZA UZITO BILA KUTUMIA NGUVU

 • Kula Chakula Cha Usiku Kabla Ya Saa Mbili Usiku

Watu wengi huwa tunalala kuanzia saa tatu mpaka saa nne, ukila chakula baada ya saa mbili usiku inamaanisha chakula hakipati muda mzuri wa kumemenyeka kabla hujalala, wachina wengi hula chakula chao cha usiku kuanzia saa kumi na mbili na nusu jioni mpaka saa mbili usiku hii hufanya chakula chao kimemenyeke vyema kabla ya wao kwenda kulala. Hii ni tip muhimu sana kama ungependa kupungua bila ya diet.

 • Chagua Vyakula Vya Kuoka Na Supu Zaidi Kuliko Vya Kukaanga

Mafuta si mazuri mwilini, kwetu wa Tanzania bila ya kula chakula cha mafuta iwe kukaanga au rost hatuoni kama tumekula hii inasababisha mafuta kugandiana mwilini na kuongezeka mwili, kwa wenzetu wao wanachagua au upendelea kula suop na vyakula vya kuoka zaidi ambavyo huwa vina mafuta kidogo mno na viungo vichache katika kupikia.

Tips Za Kupungua Uzito Ndani Ya Siku 7 – Khloe Kardashian

 • Kutumia Vyombo Vidogo

Kama huwa unaangalia movie au kufuatilia vipindi vya kichina utakuwa umegundua wachina wana kawaida ya kutumia vyombo vidogo, iwe sahani, bakuli au kikombe hii ni kutaka kuto kupakua vyakula vingi kuna msemo usemao “smaller bowls = smaller portion” lakini pia kama unavyombo vikubwa basi jitahidi kujikadiria chakula cha wastani na sio kutaka kujaza chakula kutokana na ukubwa wa chombo chako.

 • Matunda na mboga mboga

Kula mboga mboga na matunda kunasaidia pia kufanya mwili wako upungue na uwe na afya nzuri, unaweza kula mboga mboga kama main dish na kula matunda pale unapo jisikia hamu ya kula kitu kingine baada ya kula main dish hii husaidia kutokula vitu visivyo na afya kama chocolates na biscuits.

Related posts

4 Comments

 1. Where to Buy Changa DMT online Melbourne

  … [Trackback]

  […] There you will find 20909 additional Info to that Topic: afroswagga.com/dondoo/njia-6-rahisi-za-kupunguza-uzito-bila-ya-kutumia-diet/ […]

 2. Buy Burma Mushrooms for sale online Maryland,

  … [Trackback]

  […] Read More to that Topic: afroswagga.com/dondoo/njia-6-rahisi-za-kupunguza-uzito-bila-ya-kutumia-diet/ […]

 3. wachstumshormone kaufen

  … [Trackback]

  […] Read More on on that Topic: afroswagga.com/dondoo/njia-6-rahisi-za-kupunguza-uzito-bila-ya-kutumia-diet/ […]

 4. ทดลองเล่นสล็อต 2023

  … [Trackback]

  […] Find More to that Topic: afroswagga.com/dondoo/njia-6-rahisi-za-kupunguza-uzito-bila-ya-kutumia-diet/ […]

Comments are closed.