SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Proper Table Manner
Dondoo

Proper Table Manner 

Unaweza kuwa umevaa umependeza, una tembea kwa madaha na heels zako, umebeba ka clutch kazuri unanukia vyema yaani uko proper kabisa mmetoka kama ni marafiki au date ukafika uendapo halafu vitu vidogo tu vikakutia dosari, utasikia yaani msichana mrembo kapendeza ila hana proper table manners, leo tunawaletea tabia za mezani za kufanya ili tuepukane na aibu ndogondogo.

  • Subiri aliyekualika akae kabla ya wewe kukaa na unapokaa hakikisha una straight usikunje mgongo

3 Bad Posture To Fix For Confident Body Language

  • Unapokaa weka napkin kwenye mapaja yako, usiifunge shingoni
  • Weka simu pembeni au weka silent ili uweze kumsikiliza na kuongea vyema na mgeni wako, usichezee sana simu ni dharau.
  • Usiweke handbag mezani iweke nyuma ya kiti au kiti cha pembeni ambacho hakina mtu.

Je Ni Sawa Kuweka Handbag Yako Mezani?

  • Usianze kula kabla ya aliyekualika au ulie nae hakikisha unasubiri kila mtu awe na chakula na muanze kula pamoja, pia kula kwa ustaarabu don’t rush.
  • Unapotaka chakula ambacho kipo mbali na wewe omba mtu akupe, usinyanyuke au kuinua mkono kuchukua mwenyewe.
  • Unapo ombwa kitu (bakuli / sahani ya chakula) pass kuanzia kushoto kwenda kulia ili yoyote mwingine atakae taka kujiweka ajiwekee, usinyooshe mkono moja kwa moja kwa aliekuomba unless mpo wachache kama wawili au watatu.
  • Unapo ombwa chumvi au pilipili hakikisha unawapa vyote viliwi ili asiombe na kingine kama anauhitaji nacho pia
  • Unapokula hakikisha hupigi ngalo, hupigi kelele unapotafuna, usiongee wakati unachakula mdomoni, wala usitoe chakula mfano nyama kwenye meno kwa kutumia vidole na epuka kuwauliza wengine maswali wanapokuwa wanakula.

Ni matumaini yetu kuna mawili matatu umejifunza.

Related posts