SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Tatizo La Jasho La Njano Kwapani Na Suluhisho Lake
Dondoo

Tatizo La Jasho La Njano Kwapani Na Suluhisho Lake 

Sio Dar pekee bali hadi mikoani ni joto lisiloelezeka kila siku. Hii husababisha watu kutokwa jasho lisilo la kawaida n ahata mwili na nguo nzima kulowa kama vile umenyeshewa na mvua. Waweza ona wengine wakitokwa jasho makwapani ikiwa na rangi ya njano.

  • JASHO LA NJANO KWAPANI LASABABISWHA NA NINI?

Kwa kawaida jasho la binadamu lina rangi nyeupe hivyo kwa mtumiaji wa manukato iwe perfumes ama deodorants hasa zenye aluminum ndani yake, hii huchanganyikana na jasho na kusababisha rangi ya njano ambayo hutokea kwa wengi makwapani.

 

Hivyo perfumes zenye alluminium ndani yake zichanganyikapo na jasho lako hutengeneza rangi ya njano. Pia mtu apuliziapo perfumes ama deodorant kupita kiasi nayo huchangia. Wakuta mtu spray inaisha ndani ya wiki maana hupuliza nyingi utadhani ni dawa ya mbu.

Pia yaweza tokana na material ya nguo uliyovaa, sabuni uliyotumia kufukia nguo, maji unayoogea, kutokunyoa nywele kwapani na pia mchanganyiko wa kemikali za jasho lako mwilini.

NAMNA AMBAVYO UNAWEZA ZUIA TATIZO HILI

  • Ununuapo deodorants ama perfumes, kagua mchanganyiko wake kuepuka kununua zenye aluminum nyingi. Brands kama NIVEA zina deodorants special na nzuri zizuiazo tatizo hili.
  • Kabla ya kujipulizia marashi, hakikisha kwapa lako ni kavu na pia waweza itikisa deodorant yako kisha hakikisha imekauka kabla ya kuvaa nguo.
  • Ujipuliziapo marashi, tumia kiasi. Too much ya kila kitu huleta madhara. Hatupulizii kuua mende na mbu chumbani, ebho!!!
  • Pia nyoa nywele zako kwapani mara kwa mara. Misitu ya Amazon na Congo kwapani marufuku.

Imeandikwa na @willibard_jr

 

Related posts

3 Comments

  1. car locksmith

    … [Trackback]

    […] Here you will find 47587 additional Info to that Topic: afroswagga.com/dondoo/tatizo-la-jasho-la-njano-kwapani-na-suluhisho-lake/ […]

  2. 巨乳 アニメ

    … [Trackback]

    […] Here you can find 34231 more Info to that Topic: afroswagga.com/dondoo/tatizo-la-jasho-la-njano-kwapani-na-suluhisho-lake/ […]

  3. Bordeaux Wealth Advisors

    … [Trackback]

    […] Read More on that Topic: afroswagga.com/dondoo/tatizo-la-jasho-la-njano-kwapani-na-suluhisho-lake/ […]

Comments are closed.