SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

UMUHIMU WA MAHARAGWE
Afya

UMUHIMU WA MAHARAGWE 

Maharagwe imekuwa ni nafaka inayoliwa na watanzania tulio wengi hasa kutokana na kipato chetu. Lakini leo nataka nikwambia faida ipatiakanayo kwa matumizi ya nafaka hii katika afya mwanadamu. Hakika si wengi tuliokuwa tunaijua siri hii, ndio maana nimeona haja ya kushirikiana na nyinyi katika Makala hii ndogo inayohusu maharagwe. Najua tulio wengi tunayajua maharagwe na makundi yake kadhaa.
MaharagweTafiti mbalimbali zimefanywa na wataalam wa maswala ya sayansi ya lishe na kupata majibu kadhaa ambayo leo nataka na wewe msomaji wangu upate kuyafahamu ili kama hupendelei kula maharagwe basi uanze mara moja pindi tu utakapomaliza kusoma Makala hii. Zifuatazo ni faida zipatikanazo kwa kula maharagwe;Uzito

1. Kudhibiti uzito wa mwili

Katika uchunguzi wa hivi karibuni wa jarida la American Collage of Nutrition umebaini kuwa watu wanaokula maharagwe wana 22% ya kupunguza uzito wa mwili. Na wana uwezekano mkubwa wa kuwa na viuno vidogo kuliko watu wasiokula kabisa maharagwe. Maharagwe yana kiasi kikubwa cha nyuzi nyuzi zinazozoyeyuka, ambazo zinapunguza kasi ya mmeng’enyo wa chakula na kukufanya kutosikia njaa kwa muda mrefu.

2. Yanaongeza madini ya chuma

Maharagwe ni chanzo kizuri cha vitamin C ambayo yanaongeza uwezo wa mwili katika kufyonza chuma.

saratani ya titi

3. Kupunguza hatari ya kupata saratani

Katika kuangalia takwimu za lishe ya wanawake 90,630 wenye umri kati ya 26 hadi 46 katika chuo kikuu cha Havard Kitivo cha Afya ya Jamii, matokeo yalionyesha wanawake waliokuwa wakila mharagwe angalau mara mbili kwa wiki, wana asilimia 25 ya kupunguza hatari ya kupata saratani ya matiti, kulingana na  wanawake wanaokula mharagwe kwa mwezi.

 

mtoto

4. Kuthibiti mapigo ya juu ya moyo

Katika utafiti mwingine uliofanywa na wataalum wa nchini Australia, ulibaini kuwa protini iliyopo katika maharagwe na nyuzinyuzi zinazoyeyuka hudhibiti mapigo ya moyo kuwa juu.

5. Yanapunguza hatari ya Ugumba

Ulaji wa maharage upunguza athari za wanawake kupata ugumba.

 

 

Mwisho nivema kujizoeza kula walau jamii moja wapo ya maharagwe kwani zipo nyingi mno, manufaa yake ni mengi mno katika miili yetu. Asante

Imeandaliwa na

Salma Machozi
M: +255 713 002553
E: machozisalma519@gmail.com

 

Related posts

6 Comments

  1. Continue Reading

    … [Trackback]

    […] There you will find 31783 more Info to that Topic: afroswagga.com/dondoo/umuhimu-wa-maharagwe/ […]

  2. แทงบอลออนไลน์ 911

    … [Trackback]

    […] Find More Information here to that Topic: afroswagga.com/dondoo/umuhimu-wa-maharagwe/ […]

  3. weed delivery toronto

    … [Trackback]

    […] Read More here to that Topic: afroswagga.com/dondoo/umuhimu-wa-maharagwe/ […]

  4. heckler and koch pistols

    … [Trackback]

    […] Info to that Topic: afroswagga.com/dondoo/umuhimu-wa-maharagwe/ […]

  5. Automated Test Frameworks

    … [Trackback]

    […] Read More Information here on that Topic: afroswagga.com/dondoo/umuhimu-wa-maharagwe/ […]

  6. 토렌트 다운

    … [Trackback]

    […] Find More here on that Topic: afroswagga.com/dondoo/umuhimu-wa-maharagwe/ […]

Leave a Reply