Tulio wengi changamoto ya kipato na na muda imekuwa sababu kubwa linapokuja swala la mazoezi, wapo wanaokosa muda wa kuhudhuria gym, wapo wanashindwa kulipia gharama. Lakini pia tupo ambao vyote vinatushinda, sababu zipo nyingi lakini hizi mbili ndio hasa zimetufanya kuandika makala hii ya App unazohitaji kufanya mazoezi mwenyewe nyumbani.
Zipo Application nyingi za simu ambazo zimetengenezwa kwa lengo la kuwasaidia watu kama sisi ambao tunashindwa kufika gym kwa sababu moja au nyingine. Zipo Application za bure na zipo za kulipia, pia zipo ambazo ni maalum kwa ajili ya wanawake, wanaume na zipo ambazo zinaweza kutumiwa na jinsia zote.
Tumetumia Appliactions mbalimbali lakini 7M Women Workout App na Home Workout zimetuvutia zaidi. Hizi ni Application za bure na zinapatikana kwa watumiaji wa Android (Samsung, HTC, Sony, Tecno, Huawei, Infinixt…) na watumiaji wa iOS (iPhone). Baadhi ya vitu vilivyotuvutia kwenye Applications hizi ni;
Unaweza kuzitumia bila internet (offline)✈️ : Unaweza kuitumia Application hii hata simu yako ikiwa kwenye Airplane mode au hata kama kifurushi cha internet kimeisha. Hii itakuondolea usumbufu wa simu pindi unapoanza mazoezi kwasababu unaweza kuweka Airplane Mode na ukaendelea na mazoezi.
Mazoezi yamepangiliwa kulingana na lengo la mtumiaji 💪: Mazoezi yote yamepangiliwa kulingana na hitaji la mtumiaji kama (unataka kupunguza uzito unaweza kuchagua mazoezi yake). Lakini pia mazoezi yapo katika ngazi tofauti kuanzia njuka(begginer) mpaka Advanced.
Utapata repoti ya maendeleo yako ya kila siku 📋: Repoti unaipata kulingana na idadi ya mazoezi uliyoyafanya na matokeoyake katika mwili wako. Kama unafanya mazoezi ya kupunguza mwili, basi utaweza kuona kiasi cha Calories kinachokadiliwa kupungua.
Ratiba na kalenda ya mazoezi 📅: Unaweza kuseti reminder ya muda utakao kuwa unafanya mazoezi kila siku, Application itakutumia notification kila muda unapofika, hii itakusaidia kukumbusha kila muda wa maozezi unapofika.
Muda wa mazoezi ni mchache ⏰: Muda uliowekwa kwenye mazoezi ni mchache, hivyo unaweza kutumia dakika chache kila asubuhi kufanya mazoezi kabla ya kufanya jambo lolote, baada ya hapo ukaendelea na ratiba zako.
Teknolojia imeendela kuturahisishia maisha, hakuna sababu ya kutofanya mazoezi. Pamoja ya kwamba unaweza kufanya mazoezi mwenyewe, kama unayonafasi na uwezo unao wa kwenda gym, itapendeza zaidi kwasababu mbali mbali ambazo tutaziainisha kwenye andiko letu lijalo litakaloelezea umuhimu wa kufanya mazoezi gym.
Related posts
HOT TOPICS
Happiness Magese Akionyesha Wanawake Warefu Namna Ya Kuwa Stylish: Kwa wanawake warefu huwa… https://t.co/VZ1jH2zJUg
FollowHappiness Magese Akionyesha Wanawake Warefu Namna Ya Kuwa Stylish: Kwa wanawake warefu huwa… https://t.co/689j7Yjcn0
FollowSubscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
Feza Kessy Atuelezea Kuhusu Fashion & Style Zake
Feza Tadei Kessy ni Muimbaji, Muigizaji lakini pia ni mtunzi wa nyimbo lakini pia Fezza ni former beauty queen ambapo mwaka 2005 alikuwa Miss Dar City Centre, Miss Ilala & Miss Tanzania Runner up. Lakini pia alishawahi kuwepo katika Reality Tv Show – Big Brother Africa. Kwa…