SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Reviewing Enjoy Music Video By Jux ft Diamond Platnumz
Fashion Cop

Reviewing Enjoy Music Video By Jux ft Diamond Platnumz 

Kama tunavyojua kuwa juma jux na diamond platnumz kwenye swala la kutoa videos nzuri ni swala la kawaida sana. Pia usisahau kwa miaka mingi juma jux amekuwa moja kati ya wasanii wa kizazi kipya ambao wanashikilia crown katika swala la mitindo na kila siku anazidi kuimprove.

Kabla hatujaenda kureview music video basi tuwape hongera sana Juma Jux na Diamond Platnumz kwa kuwatumia watu wenye uelewa na wahusika katika video yao kwa kutumia stylist wawili ambao ni Noel Gio na Deos tylist, set designer, makeup artist na hair stylist. Jux na diamond hii ni video ya pili kufanya na inaonekana kila siku wanaimprove sana pia usisahau kuwa kuna combination ambayo imetengenezwa ya diamond Platinumz na stylist Noel Gio kwa kufanya kazi nyingi sana.

Now lets get to the review je hawa wardrobe stylist, makeup artist na hair stylist walifanya vyema?

Tulichopenda kwenye huu music video kuwa make up na hair za watu wote waliopo kwenye hiyo video walizingatia kulingana na rangi ya mtu husika. Ukiangalia nywele za Jux zipo vizuri sana yani watoto wa mjini wanasema angle imezingatiwa pia hata ukiangalia upande wa Diamond Platnumz alikuwa anabadilisha tu muonekano wa nywele zake kutokana na set .

Pia kwenye upande wa videos vixen waliandaliwa vizuri kwenye swala la make ups na nywele japo kuwa kuna makosa kidogo ambayo yalionekana kwenye upande wa baadhi ya video vixen kama walisahaulika kwa kutopakwa make ups vizuri na kuna hair pieces ambazo hatukuelewa kwanini walivalishwa hasa wale back up video vixen, na kuna ambae alivalishwa sequin pieces za club beach ila kwa upande wa wengine tulipenda mionekano yao.

Tulichopenda kuhusu hii video yani make up artist kawatendea haki sana wasanii wote walionekana kwa kuwafanyia simple make ups sio kuwakandika madude kibao usoni kwao. ukiacha vyote make up artist na hair stylist walijitaidi sana kwenye hilo swala kwa sababu walijitaidi sana kwenye kuboresha facials za watu wote walionekana kwenye hii video.

Upande wa stylist: kwa upande wa stylist yani collaboration kati ya Noel Gio na Deostylist walijitaidi sana kwenye swala la kuwavalisha wasaniii kama unavyojua now tupo kwenye trends ya colourful outfits. Nao mastylist waliamua kwenda na colourful outfits hili kufanya wasanii wawili wawe na muonekano wa kucreate attention kubwa na wawe na accent shades.

Yani Noel Gio na Deos tylist walitumia boho style au colourful style kwa sababu tofauti tofauti ikiwemo kulinks muonekano wa msaniii juu mpaka chini viwork together. Kama unavyojua kuwa Jux na Diamond walishawai kufanya music video ya sugua na hapo kama palikuwa na kibattle ambacho kila mtu alitaka kumfunika mwenzake ila kwenye music video hii ya enjoy mambo yalikuwa 50/50 kwa sababu wote walitaka kuvaa high fashion na colourful outfits bila kusahau wote walikuwa na outfits sio chini ya nne. Na tungependa kuanza na jux alivaa nguo zipi na zipi

Jux 

Kama unavyojua Jux kwa sasa amekuwa msanii ambae anapendelea sana kuvaa baggy jeans na huwa zina mtoa sana na alianza na jeans ya blue aina ya baggy jeans na vesti nyeupe, nike airforce nyeupe na glasses huku akiwa na accessories za kutosha na bado hakuonyesha kama kawa too much. Juma jux kama kawaida yake na bado akatuonyesha jinsi gani alivyo na influence katika swala la mitindo.

Then akaja na black work vest ya yenye ming’ap na suruali nyeusi na hapo akaja na dark mode ambayo imetawaliwa na jewelry na bado akavaa belts yenye jewelry bado yani alikuja na themes ya dark mode ambayo inaonyesha kuwa yeye ni mwenye thamani.

Usisahau kuwa alionekana pia kavaa aina ya vest ambayo inakibwebwe yani aliyemstylist Jux pale alithink beyond kwa kutufungua macho kwamba kibwebwe vinaweza kuvaliwa na mwanaume “yani don’t limit yourself kwenye swala la mitindo”akapendeza ila hapa alitukumbusha zamani enzi za kingwendu.

Kuna set pia alionekana akiwa ufukweni akiwa na kaptura ya blue na shirt la blue hapo alionekana kidogo na muoenekano simple kwa sababu ya aina ya location husika.

Lastly kwa upande wa Jux alivalishwa bado baggy nyekundu na work vest ya tshirt ya njano na air Jordan one hapo ndo wakaanza kuonyesha themes ya colorful outfits kama unavyoona.

Na kwa upande wa Diamond hakuwa na swala dogo yeye aliamua kwenda na colourful mwanzo mwisho kwa kuanza na full men’s jumpsuit ya blue na pia akavaa na full men jumpsuit ya pink na glasses kama kawaida yake na kuonyesha kuwa colourful outfits nowdays inatrend ulimwenguni na zinasadikika kuwa ni jumpsuit aina ya edrem.

Pia akaonekana amevaa suit nyekundu yenye urembo wa aina tofauti tofauti na glasses na hapo alionekana katika muonekano wa high fashion akiwa na colourful ways .

However, alivaaa work vest ya green na suruali nyekundu na hapo bado wakawa kwenye colourful outfits yani hii videos imejaaa colourful outfit kwa upande wa Diamond sana kuzidi hata Jux.

Tunaona Deo stylist na Noel itakuwa walishindwa kumshawishi Diamond asivae kaptura maana sio kwa miguu hiyo ila walitijaidi sana kwa sababu pamoja na miguu yake na bado akaonekana kangaa kwenye outfits yake ya colouful ways.

Kila msanii alionekana kwenye hii video kama Ommy dimpoz , Lavalava , s2kizzy wote walikuwa na colourful ways ni kitu cha kuwapongeza mastylist kwa sababu walichagua themes nzuri katika video.

Mwisho wa review music video hii ni mwanzo wa kireview video nyingine. Naomba utuambie wewe umependa nini kwenye hii video ambayo imejaa ubunifu mkubwa sana. Video Review By @GotchaTheGreatest

Unaweza kuangalia full video hapa chini

Related posts