SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

AMFVR – Umeniacha By Nuru The Light
Fashion Cop

AMFVR – Umeniacha By Nuru The Light 

Tulifanya interview na Nuru the light kuhusu kurudi kwake katika mitindo, style zake za fashion lakini pia alituambia wimbo wake mpya ameshatoa video na tukamsupport kwa kuungalia youtube oh well oh well kama Afroswagga tukasema twende tukaiangalie lakini pia tuifanyie review ya fashion zilizomo mule ndani.

Tulicho gundua mitindo uliyo tumika ni kawaida mtu yoyote anaweza kuvaa (easy to copy) lakini pia trend nyingi zimetumika kama Flare na Fur. Katika Video hii Nuru amekuwa styled na Stylist Irfan Rizwanali ambae tumepata fursa ya kuongea nae mawili matatu

Afroswagga – what’s was the story behind the outfit?
Irfan –  Tulipokuwa tukifikiria mavazi, mimi nilikuwa nawaza tu jinsi ya kumfanya awe tofauti na jinsi alivyokuwa akionekana katika video zake zilizopita. Jinsi ya kuwiana mavazi ya sasa hivi pamoja na aina ya mwili wake ili kufunika kasoro zake, pia niliwekea maanani rangi yake ya ngozi, uso wake na muhimu zaidi mandhari ya wimbo

Afroswagga -tumeona umetumia trends like flare, fur kwanini umechagua hizo?
Irfan- Kwasababu mwaka 2018 ni mwaka wa kuvunja mipaka ya frikra katika mitindo, nilijua nilitaka awe katika mavazi ya kisasa na ya kuvutia. Manyoya ni kipengele kimoja ambacho hakiwezi kamwe kupitwa na wakati. Tulitumia koti la kiofisi na kuwiana nalo na sketi ya manyoya ambayo haijawahi kuvaliwa na msanii yeyote, Pia tumetumia rangi zilizotulia ambazo ni rangi za msimu wa sasa ili zilingane na  skintone yake (rangi yake ya ngozi).

Tumetumia magauni yaliyochanua ili kumfanya aonekane na rangi na mwili mzuri na mrefu zaidi. Nguo zilikuwa na rangi ambazo zimetulia sana tukizingatia taa zilizotumika na wapiga picha na eneo ambalo video imefanyika

Afroswagga: ilikuaje kufanya kazi na Nuru?
Irfan: To be honest I never knew who Nuru was, till when I got a call from the producer a day before the shoot saying they wanted to hire me to be her Stylist.
She is one amazing lady, we connected staright away when we meet. She smart , educated and very down to earth. And the most amazing thing is she is ever ready to push the envelope. We had an amazing time working together

Afroswagga- Unawashauri nini wasanii wakiwa wanafanya video zao? wazingatie kitu gani katika mavazi?
Irfan- Wanamuziki karibia wote niliowaona au nawajua, kwa kawaida hufuata mwenendo wa kimitindo wa watu maarufu wa Hollywood. Kuhamasishwa ni kitu tofauti, lakini kuhamasishwa kwa kiwango ambacho unaanza kuiga jinsi wanavyovaa ni a Big No No. Hapana kwa kweli.
Wakati wa kupanga nguo za kuvaa kwa ajili ya wimbo, wanapaswa kukumbuka kila kipengele cha wimbo kwa undani zaidi, wimbo unahusu nini? Wimbo unahadithia nini? Je! Dhana ni nini na muhimu zaidi ni maeneo gani wanaenda kufanya video ya wimbo?

Mbali na hilo, pia msaani anatakiwa azingatie aina ya mwili wake, rangi ya ngozi na ana kasoro gani. Mambo haya yote ni muhimu sana.

Kuwa wa asili, original, tengeneza mwenendo wako mwenyewe na muhimu zaidi tumia rangi na mavazi ambayo yanaendana na wewe.

unaweza kuangalia video hapa

Related posts

1 Comment

  1. Buy DMT online New South Wales

    … [Trackback]

    […] Read More here on that Topic: afroswagga.com/fashion-cop/amfvr-umeniacha-by-nuru-the-light/ […]

Comments are closed.