SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

How Wema Sepetu & Zuchu Styled The Trench Coats In Hot Weather
Fashion Cop

How Wema Sepetu & Zuchu Styled The Trench Coats In Hot Weather 

Trench coats zilibuniwa kwa ajili ya kipindi cha baridi, kwa wale ambao bado hamjatupata tunaongelea nini trench coat’s ni zile coat ndefu zinazofika magotini. Coats hizi mara nyingi zinavaliwa kipindi cha baridi na fabric ambazo hutumika kutengenezea coats hizi ni nzito mno.

Kadri siku ambavyo zinaenda zimekuwa zikibadilishwa kwa namna moja au nyingine lakini pia fashionista wametafuta namna mbalimbali ya kuzivaa hata katika kipindi cha joto.

Hivi karibuni tumemuona muigizaji Wema Sepetu na mwanamuziki Zuchu wakiwa wamevalia vazi hili katika kazi zao, ikatufanya tujiulize hii hali ya hewa na hizi nguo zinaendana kweli?

Ukiangalia kwa umakini coats zao ni zile nyepesi sio nzito sana, rangi za coats hizi ni zile ambazo haziakisi jua kwahio hazina joto sana. Wema alivaa trench coat ya gray akiwa amematch na suruali akamalizia muonekano wake na top nyeupe.

Wakati Zuchu alivaa off white trench coat aliyo match na suruali akamalizia muonekano wake napull neck nyeupe.

Ambacho tungependa kuona Zuchu amefanya ni kuvalia vazi hili na top ambayo ina shingo ya kawaida au cami top ili kufanya vazi lionekane summer zaidi, pull neck imefanya aonekane kama amevaa vazi la winter.

Hayo ni maoni yetu tuambie kwako je umeonaje au ungependa nini kingefanyika katika vazi la Wema au Zuchu?

Related posts