SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Je Tunavuka Mipaka Kama Wedding Guest’s?
Judge Afro

Je Tunavuka Mipaka Kama Wedding Guest’s? 

Waswahili husema “Mgema akisifiwa tembo hulitia maji”, tumekuwa na tabia ya kusifia wedding guest wanaopendeza na kuwa watofauti katika harusi za watu, tunadhani sifa hizi nyingi zimesababisha wengine kuzidisha kiwango na kupitiliza mwishoe kuharibu.

Hivi karibuni kulikuwa na harusi ya hair stylist Aristotee ambapo baadhi ya watu maarufu walihudhuria katika sherehe hii, kuna baadhi ambao walionekana kupendeza na kuna wengine ambao tuliona wamepitiliza.

Moja kati ya vitu ambavyo vinashauriwa unapoenda kwenye harusi ya mtu ni kumuacha mwenye harusi aongelewe sababu ni siku yake, yaani pendeza kistaarabu na kuwa mstaabu katika sherehe ya mwenzio.

lakini pia kuzingatia aina ya mavazi tunayoyavaa yasiwe yanaonyesha sana maungo kuvuka mipaka au kuvaa vazi lenye rangi nyeupe, katika sherehe hii tuliona Masha love alivyovaa na yeye kuonekana kuongelewa zaidi kuliko wenye sherehe yao, cleavage ilikuwa too much ambapo iliondoa attention kwa wahusika.

Well ni matumaini yetu wakati mwingine hili kosa halitojirudia.

Related posts

1 Comment

  1. สล็อตเว็บตรง

    … [Trackback]

    […] Find More to that Topic: afroswagga.com/fashion-cop/judge-afro/je-tunavuka-mipaka-kama-wedding-guests/ […]

Comments are closed.