MTVMAMA Awards zime fanyika jumamosi ya tarehe 22 ambapo wa- Tanzania walikuwa nominated ambao ni Diamond, Vanessa Mdee, Ali Kiba ft Sauti Soul na Navy Kenzo ukiachana na hao kuna ambao walienda kutuwakilisha au kuwasindikiza wenzao (kuwapa support) kama Miss Tanzania Brigitte Alfred, Shilole, Naj, Baraka The Prince, Lady Jay Dee, Jokate na Sanchoka lakini pia alikuwapo Idris Sultan ambae yeye ali announce moja kati ya tuzo
kati ya hao wote walio tajwa hapo kumi na tatu ni watatu tu ambao kidogo walituvutia na mavazi yao ya siku hio wengine wote walikua so/so kawaida mno.
tuanze na ambao walivutia mbele ya maco yetu,
Sanchoka huyu ni model au video vixen (we guess we are not so sure) ila kurasa yake ya Instagram ime jaa picha za ki model model, tume penda mtoko wake wa siku hio ambao alibuniwa na mbunifu Elisha Red Label kutoka hapa hapa kwetu Tanzania. Sanchoka alivaa gauni ya metallic na ambayo ina onyesha vilivyomo ndani sheer, tume penda as ni trend kwa sasa tumesha waona watu mbalimbali akiwemo Beyonce katika mitoko ya aina hii.
Idris Sultan did us justice, alivaa suit nyeusi na white shirt ambayo ilimtosha yaani ime endana na body yake aka accessorize na clear glasses
Brigitte Alfred Former Miss Tanzania alivaa gauni jekundu ambalo halina makelele mengi, ame accessorize na silver clutch & silver accessorize, we love the look on her
Diamond Platnumz hatuwezi kusema hii ni best look yake kwa kweli, tume muona diamond katika outfit mbali mbali ambazo alishtua zaidi ya hii all in all si mbaya sana wala si nzuri sana so/so
Aika na Nahreel wa navykenzo nao walikuwepo na tupo disappointed na mavazi yao hatuna hakika na kwanini Aika ame vaa hio belt hapo kiunoni na hizo gloves,
Jokate ni mtu ambae we had much expectations on her kwamba ata pendeza mno kwenye red carpet but ika turn out vingine, gauni yake ina so much drama yani and the hair ni No
Ali Kiba na koti lake lisilo mtosha, lakini ame hojiwa jibu lake ni kwamba suit yake aliyo panga kuvaa ilichafuka so he had to change, hatudhani kama kulikua na umuhimu wa yeye kuvaa koti la suit aliweza kuvaa shirt tu na suruali aka pendeza mno. wrong move
Naj na Jojo designer wao ni mmoja we guess too much drama labda hio lace ya chini inge ondoka au inge fanywa kuwa skirt na crop top tungeelewa zaidi.
hata pa kuanza kumuelezea shishi hatujui just WORSEEEEEEEEEE
Dada Jide mmmmmmmmmmmmh, hiki kitambaa ni kama walikatiana na aika eeh? mbunifu wake sijui ali chelewa kuishona au vipi nguo haikuwa sawa na ni mbaya kiufupi
Related posts
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…