SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Nuruelly, Banana Zorro Na Kala Jeremiah Jifunzeni Kutoka Kwa Papii na Nguza Viking
Fashion Cop

Nuruelly, Banana Zorro Na Kala Jeremiah Jifunzeni Kutoka Kwa Papii na Nguza Viking 

Ikiwa tunaona tasnia ya mitindo inaanza kurudi katika heshima yake kutokana na maamuzi mbalimbali yaliyo chukuliwa hivi katibuni kama kuwa na chana cha mitindo, bi. Asya Khamsin na Hashim Lundenga kuwaachia vijana kusimamia majukwaa yao ya mitindo kuna wengine ambao bado wamekwama katika Dunia ya zamani, mitindo ya zamani.

Sio mbaya sababu kila mtu ana style yake katika swala zima la fashion lakini saa nyingine ina bidi kuangalia muda, nini kipo wakati huo na nini unataka kufanya,well seems like wasanii wa zamani wanajaribu kutoka kurudi tumeona picha kutoka kwa nuruelly akiwa na Banana Zorro na Kala Jeremiah ni kama wapo location kwa ajili ya video ya wimbo wao mpya, tuna furahi kuona wasanii wa zamani wakijumuika pamoja na kutaka kurudisha ile ladha ambayo wengine tunaimiss. Lakini pia tungefurahi zaidi kama wange jaribu ku-keep na Dunia ya sasa katika mitindo.

Hawa wasanii wa sasa wanajitahidi sana katika kuvaa japo kuna sehemu wanakosea lakini tulipo sipo kule tulipo toka, na hatutaki kurudi kule kuna wengine ambao huwa wanaangali music video kwa ajili tu watu wamependeza, na wengine wanampenda msanii na huku wengine wakipenda wimbo well kama msanii inabidi uwaridhishe mashabiki zako wa aina zote, Nuruelly, Banana Zorro na Kala Jeremiah wame tu-disappoint kwa kiasi kikubwa na tuna hope kwamba hii video ikitoka basi wawewamefanya haya marekebisho.

The suits ni za zamani mno, nani anavaa these kinds of suits with this kind of fabric these days? tulisha papita hapa zamani sana. Hizi fabric zilikuwa zinavaliwa zamani hasa kama mtu anaoa, hakuna mpangilio mzuri katika mavazi kama utaangalia kuna ambae ana tai, mwingine vifungo kafunga nusu, wengine wana mikanda wengine hawana, tunadhani bado hawajapata taarifa ya kwamba kuna stylist siku hizi, lakini swali letu kubwa ni kwamba kwanini suit ya aina moja? hata kama ni band music waangalieni basi hata saui sol jamani siku hizi tunachanganya vitu kila mtu na mavazi yake to make it more interesting.

Kwetu sisi hizi ni outfit mbaya toka mwaka uanze hasa katika upande wa wasanii wa kiume Tanzania, tukiwa tunapigia kelele wasanii wa kike kwenda gym tuna sahau wa kiume pia, Banana na Nuruelly inabidi gym iwahusu au mjaribu ku-keep up na dunia ya mitindo, Rick Ross amepungua, Dj Khaled ana jaribu kwenda gym kwanini sisi tushindwa?

Kurudi kwa wasanii kuna hitaji a big punch katika kila sekta yaani macho yote yawe kwenu lakini kama hapa tu tumeona kasoro mnadhani tutakuwa interested na kujua kinacho taka kuja? Igeni mfano wa Nguza Viking na Papii hawaja kurupuka na wao ndio walikuwa ndani kwa miaka zaidi ya kumi na wamerudi wameelewa dunia ina taka nini.

Nguza na Papii wamatafuta mbunifu ambae ameweza kuwapa mionekano ya kisasa ambayo inaendana na muziki wao.

Related posts