SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Our Two Cents On Rayvanny’s New Style “Mkupuo Style”
Fashion Cop

Our Two Cents On Rayvanny’s New Style “Mkupuo Style” 

Waswahili husema “Miluzi Mingi Humpoteza Mbwa”, Tumekuwa tukiongelea mara kwa mara kuhusu styles za wasanii wetu. Kuna wale ambao wanafanya vizuri na styles zao na kuna wale ambao wao alimradi Dunia inazunguka basi maisha yanaendelea.

Leo tunamuona msanii kutoka kundi la WCB aitwae Rayvanny, Ray Vanny hana historia nzuri sana kwetu katika swala zima la mitindo tunadhani kwake yeye hajui afanye nini kimavazi kila anachokiona anatamani kukivaa yaani he is all over hana ile personal style lakini pia hajuagi kwenda na theme, muda na hali ya hewa.

Anyways fashion ina wigo mpana inawezekana sisi tunaona si sawa lakini kuna watu ambao wao kwao Ray Vanny ni fashion icon au role model wao, leo tutaongelea huu muonekano wake mpya anaokuja nao sasa alioupa jina la mkupuo style.

May be he is ahead of time or behind it, kwa kuelewa fashion hii style aliyokuja nayo sio yake kuanzia personality yake, kazi yake na brand yake alivyoitengeneza haiendani na hii mionekano na ndio maana awali tulisema “Miluzi Mingi Humpoteza Mbwa”, yaani ana vitu vingi ambavyo vinaendelea lakini haviendani na yeye anavyoji-present.

Vanny ni mfupi mnene, kuvaa oversize nguo ni kuendelea kujididimiza na kuonekana mnene, nyimbo zake ni zile ambazo zimetulia trust us kama hii fashion angevaa shalo mwamba tusingeshangaa ni kitu ambacho anaendana nacho kwa Vanny kinachomfaa ni mavazi fulani classic yasiyo na kelele nyingi as his appearance will favor hio style, anyways who are we to judge? mates let us know maoni yako kwenye hii style mpya ya Vanny Booooy.

Related posts