SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Queen Darleen A.K.A Queen Of Fashion Crimes
Fashion Cop

Queen Darleen A.K.A Queen Of Fashion Crimes 

Leo tulikua tunaangalia biography za baadhi ya wasanii wakike Tanzania tukakutana na Biography ya Queen Darleen ambayo ni fupi kidogo imeelekeza kama Queen Darleen ni songwriter, mwanamuziki lakini pia ni Fashionista hiyo ikatufanya tujiulize mwaka upi ambao Queen Darleen aliwahi kuwa Fashionista? na kwanini aliacha kuwa Fashionista? tunachojua Queen Darleen ni Queen wa fashion crimes ni kwamba huwa ana jaribu sana au hajaribu kabisa.

Unaweza kupenda outfit yake moja kwa miezi kwa sababu zote utakazo muona nazo nyingine ni makosa, tunaweza kusema kati ya wasanii wa kike walio wahi kuwa juu kipindi hiko Queen Darleen nae yupo ametoa nyimbo mbali mbali ambazo wengi tulikuwa tunazipenda na ame weza ku-maintain nafasi yake mpaka sasa ambapo ana shirikiana na kaka yake Diamond Platnumz, ni Queen wa WCB Classic ambae hajui kutumia crown yake. Kuna wengi ambao wapo na tunaweza kusema ni wapita njia wapenzi wa wasanii kutoka WCB wanavaa vizuri sana kuliko dada mtu hii imetufanya tujiulize ni kwanini? kwanini yeye hajiweki vizuri?

Darleen unaweza kumkuta kwenye outfit nzuri ukaja kushangazwa na nywele zake, akiwa na nywele nzuri ata haribu kiatu yaani si msanii ambae utaweza kumkuta ame kamilika katika swala zima la fashion kila siku ana jipya katika ulimwengu wa mitindo ina tufanya tujiulize role model wake ni nani? maana hata lady gaga ame badilika kwa sasa, Miley Cyrus amebadilika kwanini yeye anakuwa vile vile miaka na miaka?

Huwa tunajiuliza wasanii wetu wanajua ni kiasi gani mionekano yao inaweza kuwabeba na pia kuwaangusha? mimi naweza kuona picha ya Darleen nika scrow down na mambo yangu nikamuona tu kama mtu wa kawaida lakini naweza kukutana na ya Vanessa nikamuona kapendeza nikataka kujua kama ana video mpya au wimbo mpya au hata kurepost picha yake na kuwakumbusha wengine kwamba vee bado yupo.

au hii ndo ilekuweka kichwani any publicity is a publicity even if it is a bad publicity? tunadhani ifike muda wasanii wetu wajue kwamba bad publicity watu wanakuzoea unaweza kumwambia mtu umeona picha ya Darleen alichovaa akakwambia huyo kawaida yake lakini ukamuuliza labda umemuona Jokate? akawa curious kuona jinsi alivyo vaa amependeza na yeye aige style. muda ume fika wa kujinyanyua kuwa msanii si sauti tu ingekuwa hivyo wakina Beyonce, Rihanna wasinge jisumbua na Fashion. Tunahiwaji ku-take notes kutoka kwa wenzetu.

Tupe maoni yako kupitia mitandao yetu ya kijamii facebook, Instagram & twitter 

Related posts

3 Comments

  1. DMT vape pen for sale online Australia

    … [Trackback]

    […] Find More Information here to that Topic: afroswagga.com/fashion-cop/queen-darleen-a-k-a-queen-of-fashion-crimes/ […]

  2. click this over here now

    … [Trackback]

    […] Find More here on that Topic: afroswagga.com/fashion-cop/queen-darleen-a-k-a-queen-of-fashion-crimes/ […]

  3. Mushrooms golden teacher

    … [Trackback]

    […] Find More on that Topic: afroswagga.com/fashion-cop/queen-darleen-a-k-a-queen-of-fashion-crimes/ […]

Leave a Reply