SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Wasafi Festival Looks In Songea
Fashion Cop

Wasafi Festival Looks In Songea 

Mpaka sasa wasafi festival imeshapita sehemu tatu ambapo walianza na Mtwara, wakaenda Ruangwa na week hii tumewaona wakiwa Songea, na tupo hapa kuongelea looks za recently ambayo ni Songea, utajiuliza kwanini tumeruka Ruangwa, sababu ni moja tu hakukuwa na looks za kuziongelea sana.

Songea wasanii walijiandaa, we love ambacho tumekiona, stage zilikuwa za moto makes us wonder wakimaliza Dar itakuwaje, let’s get back to the looks.

Creative looks kutoka kwa Diamond Platnumz ambae yeye alivaa kama mfungwa, G nako alikuwa na mavazi ya ki-asili huku Mbosso yeye akiwa amevalia all white looks ya taulo na vest’s wali stand out na kuwa tofauti na wengine.

Patches & Graphic Looks kutoka kwa Chegge, Lava Lava & Mh Temba, tumependa hizi looks maana zipo ki-stage zaidi, zimefanya wa stand out na waonekane kama watumbuizaji siku hio

Classy looks kutoka kwa Ommy Dimpoz, Ray Vanny & Whozu, hizi ni neat looks hawa alivaa suit na suruali za vitambaa, ikiwa Ommy na Whozu wakichagua nguo nyeusi, Rayvanny yeye alikuwa na full red

Colorful Looks kutoka kwa Darassa, Billnas na Baba Levo, yes kupanda jukwaani unaweza kujikuta umevaa sare na shabiki inabidi u-stand out moja ya kitu kinachoweza kukutofautisha na mashabiki ni chaguzi za rangi na hapa tunaona namna Darassa na Baba Levo walivyochagua nyekundu wakati Billnass yeye alikuwa na orange na white look.

Kama kuna muonekano haupo hapa ni kwamba tumesahau au haukutu-impress lakini pia tunajua tumemuacha Zuchu huyu ana article yake binafsi, tuambie muonekano upi umeupenda zaidi?

Related posts