Kwasasa wanaita being Inspired na sio ku-copy, well kuwa inspired inaruhusiwa lakini ukiwa inspired tunategemea ulete kitu ambacho kimezidi ubunifu wa awali kama sio kubadilika kabisa.
Inapotokea pale mbunifu unakuwa inspired na kukosea au kwenda tofauti na kile ambacho umekuwa inspired nacho unatupa wengine maswali kama kuiga tu umeshindwa kweli unaweza kuja na cha kwako?
Kwanini ujishushie jina au kuharibu sifa ambao umejijengea kwa wateja wako kwa kosa moja dogo? Kwa mfano tuangalie hili vazi ambalo kwa mara ya kwanza lilivaliwa na mwanamitindo Jihan Dimac kutoka kwa mbunifu Mac Couture. Hili vazi lilipostiwa sana katika mitandao ya kijamii kutokana na kwamba Jihan na Mac ndio ambao waliweza kwenda na theme katika birthday ya mama Diamond ambayo ilikuwa The Great Gatsby lakini pia she looked gorgeous in it.

Well jana tumemuona mwanamitindo Husna Maulid in exactly dress kasoro tu hili limetengenezwa na mbunifu mwingine na to make it worse halikuwa limeshonwa vizuri na halikuendana na mwili wake. Kwa upeo wetu mfupi unajua mbunifu anajua hiki kinamfaa mtu wa aina gani au namna ya kumodify kufanya kim-fit mtu wa aina nyingine, Husna mfupi hili vazi lisingeweza kumkaa vizuri, Ndio maana mbunifu akaamua kuifupisha cape lakini kwa sababu tulishaliona kwa mtu mrefu lilivyokaa na kwake ni vitu viwili tofauti.

Unaweza kuona urefu wa Jihad kushoto, vazi limemkaa vizuri length ya gauni na cape zipo sawa, wakati kulia Husna vazi limepisha urefu, gauni refu kuliko cape na finishing ya cape si nzuri.
Mbunifu unakubali vipi kutoa vazi, mteja akavaa na unaona kabisa finishing haiko vyema? Pindo la hii cape kutoka katika vazi hili la Husna Maulid ni mbaya okay umeshindwa kuwa inspired ukatoka mshono exactly na kushona pia umeshindwa?

Kama sisi tungekuwa wabunifu wa Husna tungemshauri avae hii dress bila ya cape, inge’make much sense as cape ndio imeonekana kuharibu huu muonekano, gauni ya ndani imekaa vizuri kabisa hiki kitambaa cha cape tungeongezea chini kidogo kwenye gauni liwe refu kidogo tungemaliza, wakati mwingine unahitaji kulinda status yako na kumwambia mteja ukweli kwamba hiki hakitokukaa vyema au tumeharibu tusiionyeshe jamii basi.

Tupe maoni yako wewe unaonaje hii trend ya wabunifu kucopy mavazi ya wabunifu wengine?
Related posts
5 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Info on that Topic: afroswagga.com/fashion-cop/when-copy-catting-gone-wrong/ […]
… [Trackback]
[…] Here you will find 47098 more Info to that Topic: afroswagga.com/fashion-cop/when-copy-catting-gone-wrong/ […]
… [Trackback]
[…] Read More Info here on that Topic: afroswagga.com/fashion-cop/when-copy-catting-gone-wrong/ […]
… [Trackback]
[…] Find More Info here on that Topic: afroswagga.com/fashion-cop/when-copy-catting-gone-wrong/ […]
… [Trackback]
[…] Here you can find 67440 more Info on that Topic: afroswagga.com/fashion-cop/when-copy-catting-gone-wrong/ […]