Linapokuja swala la kuvaa brand kubwa huko Nigeria huwezi kum-count out mwanamuziki Wizkid Ayo, anavaa brand kubwa kama Channel, Dolce & Gabbana, Fendi lakini his favorite brand ni Gucci. Ukipitia katika account yake ya Instagram utagundua kati ya post tatu au nne inayofuata amevaa vazi kutoka katika brand ya Gucci.

Na hivi karibuni tumemuona akiwa amebeba hii Gucci Courrier soft GG Supreme tote ambayo ilibidi tutafute thamani yake, well inauzwa Eur 1,490/- ambayo ni sawa na pesa kwa kwetu za Tanzania shilingi 3,952,686.56/-

Tumemuona akiwa ameibeba mara mbili wakati mara zote hizi alikuwa yupo safarini kwenye ndege,

Well afromates is the bag worth the investment?