Mwaka 2016 ume kuwa mwaka wenye kufurahisha na kusikitisha upande wa mitindo, siku kadhaa zilizo pita tuliona baadhi ya watu maarufu walio tuvutia kutokana na magauni yao mazuri waliyo yavaa (kama ume pitwa bonyeza hapa), lakini pia huwezi kupendeza kila siku ndio maana hata kwa wapishi kuna siku maji huzidi unga au mchele na kutoa madida, boko au uji. Hawa ni baadhi ya tulio wachagua na ni kwa sababu tu tunajua walikua na uwezo wa kufanya vizuri zaidi ya hivi.
Vanessa Mdee, Vanessa ni slayer linapo kuja swala la mavazi huwa hafikirii karibu, hatuja jua hapa kipi kilimpata hasa mpaka akavalishwa hii nguo, hii gauni ilikua nzuri bila ya hayo masponge hapo mabegani yame mfanya gauni lionekane kumvaa na kumpa muonekano mbaya juu
Shilole alikuwa katika Fiesta na ali ajiri wabunifu zipo zakwake nyingi lakini hii tumeichagua kwa sababu ilikua ya kufungulia fiesta so seen this as a first outfit tukajua kabisa hizo zinazo fuata zitakua mbaya zaidi ya hii.
Aika na Nahreeh Kutoka Navy Kenzo, Hawa ni wanamuziki na pia ni wapenzi ambao kwa Tanzania tuna weza kusema ni c0uple iliyo last muda mrefu, huwa wanavaa na kupendeza sana hatuja jua kama ni mpanio au vipi lakini katika redcarpet ya MTV Mama 2016 wali haribu na vizazi vyao.
WCB Dancers hatujui nini kilitokea hapa lakini tunacho jua boss wao ana pendeza mno
Hamisa Mobetto aliteleza katika abryanz Fashion awards na hii outfit hazija endana na tulifafanua zaidi hapa
Millen Maggese Katika BET Awards 2016
Related posts
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…