SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

PARIS FASHION WEEK HAUTE COUTURE SUMMER/SPRING SS 2018
Picha

PARIS FASHION WEEK HAUTE COUTURE SUMMER/SPRING SS 2018 

Paris Fashion Week 2018 hakika huiteka dunia maana wabunifu nguli duniani huonyesha collections zao katika jiji hili la mahaba na mitindo. hususani wiki ya Haute Couture wabunifu hutupa ladha za kipekee maana hadi uweze kuwa na a Haute Couture collection, kuna masharti lazima mbunifu ayatimize. Masharti haya ni pamoja mbunifu kuwa na workshop jijini Paris yenye kuajiri japo wafanyakazi 15 full time na kila season yaani mara mbili kwa mwaka aweze kushowcase collections jijini Paris ya mavazi ya usiku na daytime. Si kazi ndogo ati!

Mwaka huu tumevutiwa na collections za wabunifu maarufu Giambattista Valli, Chanel, Dior na Ralph & Russo.

GIAMBATTISTA VALLI

Collection nzima ilikuwa ni ya hatari. Kwa hakika twataraji kujionea Alist Hoyywood celebs wakivalia mavazi yake maana magauni yake yamebuniwa kufaa red carpets nyingi. Chiffon imetumika kwa wingi pia zile tulles ziliteka macho ya wengi. Tayari tumejionea model Kendall Jenner akivaa nguo za mbunifu huyu alipohudhuria tuzo za Golden Globes mwaka huu.

 

CHANEL

Collection ilikuwa na suits, Chanel way pia short gowns ambapo rose, pink na white satin pamoja floral dressed zilitawala. Pia tulijionea floral crystals. Collection hii Karl Lagerflied alisema angependa kuwafikia na kuwaona young girl wengi wakipendeza na Chanel.

DIOR

Collection hii likuwa ni mchanganiko mzuri wa art na fashion. Pia models walionekana wakivalia head pieces za kitofauti ambapo mbunifu mkuu toka Doir, Maria Grazia Chiuri alielezea kuwa head pieces hizi zilimark a mask ball room  party amabyo pia alifanya baada ya show yake hiyo ya mavazi. Tulipenda p[ia rangi zilizotumika na kupangiliwa,  nyeusi na nyeupe zikitawala.

RALPH & RUSSO

Toka 2007 kuanzishwa kwake hadi sasa  wemeveza kuiteka dunia ya ubunifu kwa kazi zao. Mwaka huu collection yako iliweza kuwa ya rangi za kuvutia na kung’aa wakitupa shades of red, yellow, violet, na pink. Ila funga kazi ilikuwa ni gauni la harusi ambalo blogger toka Brazil Camila Coelho aliweza teka wengi alipopita nalo katika runway.

Imeandikwa na @willibard_jr

Related posts

1 Comment

  1. chocolate golden balls near me

    … [Trackback]

    […] Info to that Topic: afroswagga.com/fashion-week/paris-fashion-week-haute-couture-summer-spring-ss-2018/ […]

Comments are closed.