SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

ANA KWA ANA NA FROLINYAH
Ana Kwa Ana

ANA KWA ANA NA FROLINYAH 

Ana kwa ana ni kipengele ambacho huwa tuna fanya mahojiano na wanamitindo, wabunifu au mtu yoyote anaye jihusisha na maswala ya mitindo Tanzania, na leo tume kutana na mwanadada Florinyahdesigns ambae ubunifu wake ni wa kitofauti kidogo. Florinya ana tumia uzi na sindano kutengeneza Urembo na haya ni mahojiano kati yetu na Florinyah.
florinya3
Afroswagga-Florinyah Ni Nani?
Frorinyah- Florinyah maana yake ni Flora kwa kiportuguese (Jina language). Florinyah ni mbunifu wa kazi za mikono anaetengeneza vitu (accessories especially) kwa kutumia “Ufumaji”. Kazi zetu zinahusika na utumiaji wa nyuzi, sindano, na vitu mbali mbali (It all depends hah).I love my name and so I thought of gracing my business with the same name
Afroswagga-Ameanza lini huu ubunifu?
Frorinyah- Ufumaji nimejifunza kutoka kwa mama yangu, toka nikiwa na miaka 4. Mama yangu ni mshonaji na mfumaji mwenye experience ya muda mrefu sana. Alikuwa akifuma kazi zake atanipa sindano yangu na nyuzi na kuniambia nifume ‘chain’ ambayo ataitumia katika kuunganisha kwenye vitambaa vyake. Banda ya kumaliza chuo 2011 (UK) niliamua kujikumbushia kufuma huku nikiwa nimeajiriwa. Nikiwa najitengenezea accessories na vitu vidogo vidogo ndipo niliporudi Tanzania with the help and assistance from my best friend Edna Ndibs nikaamua kuingia kwenye tasnia ya Fashion as an Accessory Designer.
Afroswagga- Style Yako Inaitwaje?
Frorinyah- Style yangu ni ya ufumaji yaani “crochet” kwa lugha ya kigeni (English). Kama utakumbuka miaka ya nyuma wamama wengi walikuwa wanajishughulisha Sana na kazi za mikono. Mimi binafsi mama yangu alikuwa akifuma sana seti za vitambaa pamoja na ufundi wa cherehani. Mimi nilikuwa namsaidia kufuma “chain” na yeye alikuwa akizitumia katika kuunganishia kwenye patterns nyingine. So style yangu inahusisha : Kufuma – utumiaji wa nyuzi na sindano (crochet needle).
florinya2
Afroswagga- Kwa nini ubunifu wa kufuma?
Frorinyah- Kwasababu ni ujuzi ambao umesahaulika Sana. Ni ujuzi ambao unaweza kuutumia katika vitu vingi mno. Na ni ujuzi ambao ni rahisi sana kumfundisha mtu na hauhitaji ustadi mwingi. Just a few basic things and ideas and your good to go. Ni ujuzi asilia, na nikipaji, nnachoamini mwenyezi Mungu amenipa niweze kuelimisha wengine kwa kupitia kazi zangu.
Afroswagga-Matatizo gani ambayo umesha wahi kukumbana nayo katika hii fani yako?
Frorinyah-  Kwanza kabisa kuweza kumwelewesha mtu kuwa kazi zangu ni “ufumaji”. Sio wengi wanaelewa ninachokifanya. Nilipoanza iliniwia vigumu hasa kuwashawishi watu kuwa mimi nafuma na si tumii mashine. Kila kazi unayoiona kwenye kurasa zangu ni mimi mwenyewe na usaidizi wa mama yangu. Ufumaji wa accessories sio ubunifu unaofahamika Tanzania au kukuta watu/mtu anafanya kazi Kama yangu. Tumezoea kuona masweta, kazi za kimaasai, etc. Sasa mwanzaoni hata sasa bado watu hawajaelewa vizuri but naamini ipo siku kazi yangu itajitangaza yenyewe. Na shukrani kwa wale wote wanaoitambua kazi yangu na kunisupport. Asanteni Sana – Mbarikiwe.
florinya6
Afroswagga- Mara yako ya kwanza kushowcase ubunifu wako ilikuwa lini na wapi?
Frorinyah-  Mara ya kwanza kabisa kushowcase ilikuwa ni JAMBO FASHION AFFAIR – 6th June,2015 mjini Arusha. Ambapo nilishowcase collection yangu ya kwanza iitwayo “Shades Of Red And Blue (2015)”. This was the best day of my life in 2015, sitakaa niisahau hah….and I thank God for that blessing.
Afroswagga- Nini/Nani amekuinspire kwenye ubunifu?
Frorinya-  Well my mom is my inspiration. Yeye ndie alienifundisha na kuniinspire kwenye ufumaji na pia ubunifu wa styles tofauti tofauti. She is a pro I should say hah…..Amenifundisha na bado ananifundisha patterns (styles) nyingi za ufumaji na ananisaidia sana katika kufuma na kuniadvice. Am blessed for having her.
Afroswagga- Una mpango wa kufanya ubunifu wa aina nyingine zaidi ya huu?
Frorinyah-   Kwa kweli Kwa sasa siwezi kusema ndio au hapana. Simply because, kwenye ufumaji hauko limited kufanya kitu kimoja tu. But at the moment na focus on my accessories mpaka hapo baadae kidogo ndo ntaweza ku branch out kwenye vitu vingine. So at the moment am working hard on bringing the awareness of what I do first then tutaona what the future holds na ku branch out but under the same crochet roof.
florinya4
Afroswagga- Malengo yako ya baadae ni nini?
Frorinyah-  Malengo yangu ya baadae nikufikia level ya kimataifa. Kufanya Florinyah Designs kujulikana sio ndani ya Tanzania tu bali na nje ya Africa na ulimwengu mzima. Na pia kushiriki katika international platforms. Moreover, kuanzisha sehemu ambayo vijana au mtu yeyote wataweza kujifunza ufumaji.
 Afroswagga- Unaambia nini waTanzania?
Frorinyah-  Well, watanzania especially vijana, napenda kuwaambia kuwa tusitegemee sana ajira za kuajiriwa. Tujifunze kufukiria nje ya box – Think outside the box . Hakuna kitu chochote kirahisi hapa duniani. Tujifunze kujitegemea na kufikia malengo kwa kujituma na kuwa na self discipline and determination. Kuna fursa nyingi mno na sio mpaka uwe na mtaji wa mamillions – Hapana….Chochote kitu kiinvest na utaona mafanikio yake. Na pia tuwe na moyo wa kujituma na sio kutafuta short cuts in life because if it was easier to achieve trust me it will be very easy to loose it,be original, be creative and don’t copy. Lastly, muweke Mungu katika kila jambo.
Unaweza kumfollow instagram kuona kazi zake nyingine @florinyahdesigns
ASANTE

Related posts

3 Comments

 1. best passive income

  … [Trackback]

  […] Read More on that Topic: afroswagga.com/habari/ana-kwa-ana-na-frolinya/ […]

 2. from this source

  … [Trackback]

  […] Find More Info here on that Topic: afroswagga.com/habari/ana-kwa-ana-na-frolinya/ […]

 3. mushroom gummies colorado

  … [Trackback]

  […] Here you can find 51611 more Information on that Topic: afroswagga.com/habari/ana-kwa-ana-na-frolinya/ […]

Leave a Reply