SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Barua Ya Wazi Kwa Waandaji Wa Miss Tanzania
Habari

Barua Ya Wazi Kwa Waandaji Wa Miss Tanzania 

Ni mwaka mwingine tena tunaenda Sanya China katika Miss World na kurudi na experience badala ya ushindi, well kwanini hii inatokea miaka hii tu? miaka iliyopita kulikuwa na nini mpaka wakina Nancy Sumari walikuwa wanashinda? Nini cha tofauti na kwanini hakirekebishwi? Tumeridhika na experience au we don’t care any more? Inawezekana mamiss wanajitahidi sana katika maswali na kujiandaa lakini nini kinatuangusha? Ukifikiria kiundani zaidi zamani hakukuwa hata na mitandao ya kusema kuomba wa Tanzania wampigie kura miss au taarifa zifike kirahisi tofauti na sasa ambapo we have all the means za kuleta ushindi nyumbani ni nini kinatuangusha?

Hivi ni vitu muhimu tulicho notice mwaka huu,

  • Management

 

Ukiangalia kwenye post za miss Tanzania watanzania wengi wamekuwa wakilalamikia management ya miss Tanzania mwaka huu, wengi wanalalamika wakitoa ushauri wao wana blockiwa au kujibiwa vibaya na management hio, funny right? una m-block vipi mtanzania ambae anakupa ushauri wa namna ya kufanya miss wetu arudi na ushindi? una mjibuje vibaya mtanzania ambae unamuomba apige kura miss wake ashinde? They say kubali wito kataa neno, msikilize mtu mwambie tutalifanyia kazi hata kama hutolifanyia lakini mridhishe for a person to take his/her time kukuandikia nini kifanyike ni ishara tosha bado wanaimani na hili shindano na wanataka ushindi urudi nyumbani, then anakuja kupata tofauti na anachotegemea kesho umuombe apige kura, hatopiga na hili ni moja kubwa lililotuangusha mwaka huu.

Maoni yetu kwa washiriki wa Miss Tanzania 2018

  • Muda 

Hili bado linabidi kufanyiwa kazi, Miss amechaguliwa September halafu November kaenda kushiriki Miss World amepata mwezi mmoja tu wa kujiandaa, hapo labda ni kufundishwa aendapo miss World lakini hajapata muda wa kujulikana na jamii, mpaka jamii ishawishike kumpigia kura tofauti na wenzetu wanachagua ma-miss mapema na kuwapa muda wa kujulikana na jamii ili iweze kushawishika kumpigia kura

 

  • Awareness 

Tuwe tu wakweli watu hawakuwa wanajua mfumo wa kupiga kura, hakukua na awareness yakutosha katika upigaji kura lakini pia katika matangazo kwamba kuna miss anahitaji apigiwe kura na hii tunarudi palepale kutokana na muda kuwa mchache watu hawakuweza kutambulishwa miss wao, Miss hakufanya hata kazi za kijamii na wala hatukujua agenda yake ya beauty with purpose mpaka dakika za mwisho, lakini pia majibu mabaya ya muandaaji yalifanya hata wale wachache wenye uelewa kutokupiga kura.

 

Hashimu Lundenga Aachia Kiti Na Kimerithiwa na Miss Tanzania 1998, Basilla Mwanukuzi

  • Kura Na Maelezo Ya Uongo

wrong information, information zilikuwa juu juu tu hakukua na mtu wa kutoa information za kwamba njia ya sahihi ni hii, watu wanashare link sio zenyewe na hakuna mtu ana speak up kwamba hapana hii sio sawa wale wachache waliokuwa wanapiga kura nao wakaenda kupiga kura kusiko sahihi.

  • Kutokushirikiana na Mamiss Walio Pita

Bado tupo kwenye alama ya kiulizo kwanini former miss Tanzania hawashirikishwi katika kumuandaa current miss Tanzania lakini pia katika kushawishi watanzania wapige kura ukiangalia former miss Tanzania wanawafuasi wengi sana katika social net work kama wangetumika vizuri kwa kupewa information nzuri za namna ambavyo tunaweza kupiga kura toka siku ya kwanza, tunauhakika tungeweza kujizolea kura nyingi tu. Lakini baada ya kuona hali tete dakika ya mwisho ndio unaanza kuona post mbili tatu kutoka kwa mamiss waliopita, hii pia imeonekana kwa fashion bloggers, models na kila ambae yupo kwenye fashion industry we need to lift each other up, mmoja anapokuwa kwenye shindano kubwa kama hili haijalishi upo upande gani wa industry we need to support that person on a hundred.

Well let’s hope for a change mwakani hopeful tutaona mabadiliko.

Related posts

3 Comments

  1. Plantation Shutters

    … [Trackback]

    […] Information on that Topic: afroswagga.com/habari/barua-ya-wazi-kwa-waandaji-wa-miss-tanzania/ […]

  2. all slot auto wallet

    … [Trackback]

    […] There you will find 31035 more Information on that Topic: afroswagga.com/habari/barua-ya-wazi-kwa-waandaji-wa-miss-tanzania/ […]

  3. cartel & co

    … [Trackback]

    […] Info to that Topic: afroswagga.com/habari/barua-ya-wazi-kwa-waandaji-wa-miss-tanzania/ […]

Comments are closed.