SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Dondoo 5 Za Mitindo Kwa Watu Wanene
Habari

Dondoo 5 Za Mitindo Kwa Watu Wanene 

Miili imekuwa kisingizio cha wengi kutokuvaa na kupendeza, lakini kumbe kila mmoja wetu anaweza kuvaa na akapendeza inatakiwa tu uujulie mwili wako wa aina gani na mavazi yapi yanakufaa, kama ungependa kujua zaidi kuhusu aina ya mwili wako na mavazi yapi yana kufaa tunashare link hapo chini ukasome.

Lakini hizi ni Dondoo 5 ambazo tumekuandalia kiujumla kama una mwili mnene zinaweza kukufaa

  • Crop It 

Vaa crop top yako na high waist pants au skirt kutengeneza shape, high waist trouser zinakusaidia kukupa muonekano wa kiuno chembamba.

  • Flare it

Flared pant will never go out of style, ni vyema ukawa nayo katika kabati lako. Hakikisha unaivaa na top fupi au chomekea kukupa balance ya mwili wako na outfit yako, kama si mpenzi wa suruali, kuna flare dresses pia.

  • Wrap it up

Wekeza katika wrap dresses au wrap tops, Wrap dress ni kama flare pants ni vyema ukawa nazo katika kabati lako, husaidia kutenganisha kifua na kiuno na kukutengenezea muonekano mzuri wa mwili wako.

  • Chagua Material Sahihi Ya Mavazi Yako

Kama wewe ni mpenzi wa mavazi yenye material membamba inabidi uachane nayo na kuanza kununua mavazi ambayo yana material nene kidogo kama, spandex na neoprene material. Sababu material haya yanakufanya uonekane slim kuliko ambavyo upo.

  • Usifiche Mwili Wako

Wengi wenye miili hii huwa tunachagua mavazi makubwa kuliko sisi, tukidhani zinatupa muonekano mzuri lakini kumbe zinazidi kutuficha na kufanya miili yetu izidi kuonekana mikubwa, badala yake chagua mavazi ambayo yana kufit vyema na kuonyesha sehemu ambazo unadhani zina favor mwili wako. Yaani kama una miguu mizuri basi vaa nguo inayokufit vyema lakini fupi ionyeshayo miguu, kama ni mabega basi fanya hivyo pia n.k

Picha zote zilizotumika ni za @ms.chicca_bwase

 

Related posts

1 Comment

  1. รับทำบัญชี

    … [Trackback]

    […] Read More Info here to that Topic: afroswagga.com/habari/dondoo-5-za-mitindo-kwa-watu-wanene/ […]

Comments are closed.