Ikiwa imesalia takribani siku moja tu, kufanyika kwa onesho ambalo ni la aina yake katika ulimwengu wa sanaa na ubunifu wa mavazi ‘Fashion For Peace’. AfroSwagga ilipata fulsa ya kufanya mahojiano na Maryam Ngwangwa, Meneja Mahusiano wa onesho hilo alisema maandalizi yanaendelea vizuri huku kila mbunifu akiwa yupo tayari kabisa kwa kutuonyesha maajabu yake siku ya onesho hilo, Maryam aliieleza AfroSwaggga kuwa watakuwa na jumla ya mamodel 20 ambao kati yao mamodel 12 watakuwa Wakike na mamodel 8 Wakiume. Maandalizi ya jukwaa pia yanaendelea vizuri na mpaka sasa wamefanikiwa kuuza jumla ya tickets 300, ukitoa zile ambazo vitagawiwa kama zawadi kwa washindi watano watakao patikana kupitia shindano linaendelea mpaka sasa katika mtandao wa Instagram kwa kutumia hashtag ya #fashion4peace. Alisema ” Tumetoa tickets 5, 2 zikiwa za VIP na 3 zikiwa za kawaida kwa washindi watakaopatikana instagram”. Mbali na hayo Fashion For Peace itapambwa na burudani kutoka katika kikundi cha ngoma za asili cha Simba Chawene. Maryam alimalizia kwa kusema kuwa tickets bado zipo katika vituo vilivyotangazwa hivyo watu waendelee kujitokeza kununua.
Related posts
3 Comments
Leave a Reply Cancel reply
You must be logged in to post a comment.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Read More Information here on that Topic: afroswagga.com/habari/fashion-for-peace-mambo-moto-moto/ […]
… [Trackback]
[…] Find More Information here to that Topic: afroswagga.com/habari/fashion-for-peace-mambo-moto-moto/ […]
… [Trackback]
[…] Read More here to that Topic: afroswagga.com/habari/fashion-for-peace-mambo-moto-moto/ […]