SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Fashion Video Review – Salome By Diamond Vs Raymond
Habari

Fashion Video Review – Salome By Diamond Vs Raymond 

‘Kweli iliyo uchungu si uwongo ulio mtamu’ Diamond Platnumz.

Kadri miaka inavyokwenda tumeendelea kuona kusifiana uwongo, na uwongo umeonekana kuwa mtamu zaidi ila uchungu umegeuka katika upande wa ukweli na wengi kuona ukweli ni mbaya katika maisha yao.

Hii inafanya kuona wasanii wengi wapo sahihi katika mambo mengi, ila katika uhalisia ni wazi wamekuwa wakipotoka katika mambo mengi. Afroswagga tumejikita zaidi katika upande wa mavazi (Fashion) na daima tunasimama katika ukweli sisi sio watu wa uwongo mtamu kama walivyo wengine.

IMG_20160918_214903_442

Kila mmoja amekuwa akiongea juu ya wimbo wa Salome ambao ni wimbo mpya wa Diamond Platnumz, kiuhalisia ni wimbo mzuri.

Ila katika upande wa video ni wazi umekuwa si upande mzuri kama ambavyo wengi wao wenye uwongo ulio mtamu wanavyoendelea kuhubiri tangu kutoka kwa wimbo huo.

Sisi tunafananisha video hiyo na msemo usemao “Shoka lisilo na mpini halichanji kuni” Tukiwa na maana muziki ni njia moja wapo ya kutangaza vitu vingi katika nchi husika, vitu hivyo vyaweza kuwa mavazi, utamaduni, vyakula, na mengine mengi.

diamond-platnumz-ft-rayvanny-salome_9494405-11670_1920x1080

Katika upande wa Diamond kwenye video ya Salome tumeona akiwa amevaa mavazi ya Nigeria. Hatuwezi kusifu juu ya muonekano wake katika video hiyo maana nguvu aliyotumia kutangaza mavazi ya Nigeria ni wa hali ya juu.

Ikumbukwe leo hii ukiona tu mavazi ya Nigeria, Uganda, Ghana hizo ni baadhi ya nchi ambazo wasanii na watu wao maarufu wamekuwa wakitumia sanaa zao katika kutangaza mavazi yao.

Tunafahamu kama nchi yetu hatuna vazi la taifa ila yapo mavazi ambayo ukivaa unaonekana wewe ni mtanzania, hivyo ni vyema Diamond Platnumz kuamka kifikra wimbo kama Salome ilipaswa kuutendea haki kwenye video kama ambavyo aliutendea haki mmiliki halali Saida Karoli

imeandikwa na @batro15

tupe Maoni Yako kupitia

Instagram – AFroswagga

Twitter – Afroswaggatz

Facebook – Afroswaggamag

Related posts