SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Flaviana Matata Afunguka Kuhusu Kuvunjika Kwa Ndoa Yake, Jackie Cliff Arudi Uraiani, Budget Ya Harusi Ya Aristoste + More
Afro Weekly Highlights

Flaviana Matata Afunguka Kuhusu Kuvunjika Kwa Ndoa Yake, Jackie Cliff Arudi Uraiani, Budget Ya Harusi Ya Aristoste + More 

Week nyingine imeisha na huwatunajua ni lazima kuwe na jambo la kuongelea, well week hii zilizoonekana kushika masikio ya watu kwenye mitandao ya kijamii ni pamoja na mwanamitindo Flaviana Matata kufunguka kuvunjika kwa ndoa yake.

Flaviana Matata alifunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu Deogratius Massawe  mwaka 2015, Week hii Flaviana alipost kwenye account yake ya Instagram na kusema kwamba ndoa hio ilivunjika toka mwaka 2019. Flaviana alifunguka haya baada ya mwanamuziki Adele kufunguka kuhusu kuvunjika kwa ndoa yake kwenye interview yake na Oprah. Flaviana aliongelea magumu aliyopitia baada ya ndoa yake kuvunjika na kuitaka jamii kuacha kuwalaumu wanawake pale ambapo ndoa zikivunjika.

Kwenye habari nyingine Fashionista Jackie Cliff amerudi uraiani baada ya kutumikia kifungo cha miaka minane huko Nchini China, ikumbukwe Jacqueline alikamatwa na madawa ya kulevya mwaka 2013. Jacqueline alipost picha yake katika account yake ya Instagram na kusema ametumiss. Ukiachana kurudi Jacqueline amefungua ukurasa mpya wa instagram ambao mpaka sasa unasiku 5 tu na amejipatia followers 101k yaani laki moja na elfu moja.

Kubwa lingine lililoonekana ku-make headline’s ni budget ya harusi ya hair stylist Aristotee ambapo anafunga ndoa jumamosi ya leo, imeonekana budget ya harusi nzima ni Tsh 180,000,000/- ikiwa gauni la bibi harusi limegharimu 6,000,000/- huku suit ya bwana harusi ni 4,000,000/- ukiachana na mavazi vingine vilivyoonekana kuongelewa zaidi ni hii budget ya vinywaji, ua la bibi harusi ku-gharimu 500,000 na kutumia helicopter katika harusi yao, well truth or not tutajionea leo.

As we once said unisex fashion inashika hatamu Nchini kwetu, week hii tumewaona mwanamuziki Kayumba pamoja na Barnaba wakiwa in unisex style, Kayumba yeye alivalia zake blonde bob wig huku Barnaba akiwa kwenye leather min dress.

Barnaba & Elly Fire In Unisex Fashion 

Mitindo Ya Unisex Inavyokuja Taratibu Nchini Tanzania

well hizo ndio habari 4 zilizo-trend week hii kwa upande wa mitindo Tanzania, tuambie ipi imekushtua ipi imekufuraisha na ipi umeona mmmh hii isiendelee.

unaweza kutembelea katika account zetu za mitandao ya kijamii kwa update za habari za mitindo kila siku

instagram – @afroswagga

Twitter – @afroswaggatz

Related posts