SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Gumzo Juu Ya Mavazi Ya Miss Kyerwa 2021
Habari

Gumzo Juu Ya Mavazi Ya Miss Kyerwa 2021 

Zulfa Yazid Suleiman (20) hivi karibuni alishinda kuwa Miss Kyelwa 2021, Zulfa amezua gumzo katika mitandao ya kijamii kutokana na uchaguzi wake wa mavazi aliyoyavaa katika uzinduzi wa Jengo La Mkuu Wa Wilaya ya Kyerwa.

Katika uzinduzi huo, Zulfa alichagua kuvaaa ripped jeans, stripped tshirt na raba, kitu ambacho kilizua gumzo kutokana na kwamba mavazi haya hayaendani na tukio alilokwenda kuhudhuria. Tulitegemea kumuona akiwa smart kimavazi kutokana na taji lake alilotunukiwa lakini pia ukiangalia wengine wote waliohudhuria tukio hili walikua wamevalia kuendana na tukio huku wengi wao wakiwa na umri mkubwa kuliko yeye.

Hii imesababisha tujiulize Je kosa ni la Zulfa au waandaaji na management yake? Kwanini aliruhusiwa kutoka akiwa amevaa mavazi haya kwenda kwenye tukio kubwa kama hili? Je Zulfa mwenyewe kwakupenda kwake urembo mpaka kwenda kushiriki Miss Kyerwa na kushinda taji hilo, hajui ni mavazi ya aina gani yavaliwe wapi mpaka akamua kuvaa mavazi haya?

Ukiangalia vizuri utagundua Zulfa amevaa sash zake zote mbili tena kwa mtindo wa X, Je hakufundishwa namna nzuri ya kuvaa hizi sash? Well tunadhani kupitia kwa Zulfa wengine pia watajifunza lakini pia management ya hawa warembo tungependa muwe mnawapa warembo wetu taarifa mapema na namna wanatakiwa wajiweke ikiwa wanabeba sura ya sehemu husika.

#Afromates tuambie hapo chini unadhani nani wa kulaumiwa?

Related posts

4 Comments

  1. Plantation Shutters

    … [Trackback]

    […] Information to that Topic: afroswagga.com/habari/gumzo-juu-ya-mavazi-ya-miss-kyerwa-2021/ […]

  2. emergency call out

    … [Trackback]

    […] Find More Info here on that Topic: afroswagga.com/habari/gumzo-juu-ya-mavazi-ya-miss-kyerwa-2021/ […]

  3. edible gold chocolate bar

    … [Trackback]

    […] Find More Info here to that Topic: afroswagga.com/habari/gumzo-juu-ya-mavazi-ya-miss-kyerwa-2021/ […]

  4. useful content

    … [Trackback]

    […] Here you can find 1974 additional Info to that Topic: afroswagga.com/habari/gumzo-juu-ya-mavazi-ya-miss-kyerwa-2021/ […]

Comments are closed.