SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Hashimu Lundenga Aachia Kiti Na Kimerithiwa na Miss Tanzania 1998, Basilla Mwanukuzi
Habari

Hashimu Lundenga Aachia Kiti Na Kimerithiwa na Miss Tanzania 1998, Basilla Mwanukuzi 

We didn’t see this coming but we are glad kwamba finally yametokea na kuwezekana, aliye kuwa muandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Bw. Hashim Lundenga ameamua kuachana na kuandaa shindano hilo baada ya kuona shindano lina suasua na yeye umri umepita ana timiza miaka 61 mwaka huu na kwamba ameona awaachie vijana, well this is news. Tuna furahi kuona vijana wanapata fursa ya kuendeleza hili gurudumu la mitindo alianza dada Asya Khamsin na Lady In Red Fashion Show na sasa ni Lundenga.

Tukawa tunajiuliza je hakutakuwa na shindano tena? gladly hili nalo limejibiwa mapema kabla hata ya figisufigisu kuanza, Aliye kuwa Miss Tanzania 1998 Bi Basila Mwanukuzi ndiye aliye chukua kiti cha Lundenga na ndiye atakuwa akiandaa shindano hilo, We are so happy hili limetokea. kwanini tumefurahi kwanza kabisa ukiachana na Basila kuwa alikuwa Miss Tanzania bali pia ni kwamba ni mwanamke, tuna furahi kuona Miss Tanzania itaongozwa na mwanamke giving women opportunity katika vitu vikubwa katika Nchi kama hivi ni kitu kizuri kinawapa matumaini wanawake wengine huko nje na hata wale waliokufa moyo kushiriki hili shindano sasa watashiriki.

Lakipi pia Basila ana experience, alisha wahi kuwa Miss Tanzania inamaanisha vingi anavijua, amesha shiriki Miss World anajua wapi alikosea wapi panatakiwa kuwa vipi, jinsi ambavyo miss anatakiwa kuwa as tunaona ma Miss wetu wa sasa hivi ni kubishana tu huko kwenye mitandano wakati wao wa zamani wanamaisha yao mazuri tu, tuna dhani atarudisha hadhi ya shindano hili.

Basila ni mpenda mitindo na ana tangaza wabunifu wa Tanzania, ukiachana na kwamba amemaliza muda wake wa Miss Tanzania, Basila bado ana jibeba kama Miss Tanzania anapenda mitindo lakini pia ni moja kati ya wale wa chache wanaopenda kuvaa mavazi ya wabunifu wetu so tuna uhakika kwamba Miss Tanzania atakae patikana katika mikono yako sio tu atatangaza Nchi kupitia yeye bali pia atawatangaza wabunifu wetu.

 

Wapi inabidi Basila abadilishe na Akazie? 

Tungependa kuona vijana wakishirishwa zaidi katika hili shindano, tuna damu changa nyingi ambazo zinafanya mapinduzi huko nje za Nchi, Kina Hapiness Magesse, Miriam Odemba, washirishwe stylist kama Rio Paul, Swalha Msabaha na wengine wengi hii itasaidia sana kurudisha hadhi ya shindano na kuanza fresh from scratch, inaitwa kusaidiana.

Kuwahi kufanya shindano, hili ni muhimu ili kuondoa ile excuse ya kwamba tumechelewa kujiandaa, hakukua na sponsors, hamna support na excuse nyingine nyingi. Shindano liwahi kufanyika miss apate kujiandaa, watu wapate kumjua hata akienda huko akaomba kura watu wapige. Miss arudishwe kufanya shughuli za kijamii, kusaidia jamii siku hizi Miss akishachaguliwa basi hatuoni cha maana anacho kifanya, tungependa kuona hali ikirudi kama ilivyo kuwa zamani tumtambue Miss wetu na mchango wake kwetu.

Zawadi, Miss apate zawadi aliyo ahidiwa mapema kati ya mambo ambayo yanawavunjisha moyo wasichana wengi kushiriki shindano hili moja wapo ni hili la figisu za zawadi tungependa kuona linaondolewa na Miss apate kile anacho shahili, all in all tumependa kilicho fanyika tunaomba iwe kheri na shindano liende vizuri tutakuwa hapa katika kila step inakayo chukuliwa.

 

 

Related posts

2 Comments

  1. can you download a video from youtube

    … [Trackback]

    […] Read More on on that Topic: afroswagga.com/habari/hashimu-lundenga-aachia-kiti-na-kimerithiwa-na-miss-tanzania-1998-basilla-mwanukuzi/ […]

  2. hawaiian magic mushrooms

    … [Trackback]

    […] Information on that Topic: afroswagga.com/habari/hashimu-lundenga-aachia-kiti-na-kimerithiwa-na-miss-tanzania-1998-basilla-mwanukuzi/ […]

Comments are closed.