SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

JINSI GUCCI WALIVYO TEMBELEA NYOTA
Habari

JINSI GUCCI WALIVYO TEMBELEA NYOTA 

Kila siku huwa tuna sema wabunifu wetu ni wazuri lakini hawajui kucheza na wakati tunadhani ni muda sasa wa wao kujifunza kutoka kwa wenzetu, moja kati ya wabunifu ambao tumeona wame tumia akili ya ziada ni Gucci, ni kampuni ya zamani na pia ni kampuni kubwa sana duniani lakini haija pumzika kusema hapa tume fika hapana, kila wanapo ona msanii au mtu maarufu kavaa kitu chao wana hakikisha hicho kitu kina shout.

Kama tukio la hivi karibuni, ambapo Beyoce alihudhuria the NBA All Star Game akiwa ame valia kimono kutoka kwa mbunifu Gucci chenye thamani ya $21,945 ina weza ikawa kawaida kwake lakini kwa wengine si kawaida. Kimono hiko thamani yake ni TSH 48,281,200 wengine walitengenezea meme kwamba Beyonce kavaa nguo yenye thamani ya kununua gari which is true,

Lakini kuna hii nguo unavyo iona ukiikuta mtumbani huinunui, lakini thamni yake kubwa na hapo kuna mawili ina wezekana beyo kanunua kweli, Lakini pia ina wezekana Gucci walimpa aivae katika hio show ilikujitangaza na ni strategy nzuri katika biashara kwa sasa kila mtu anae mfuatilia Beyonce anaijua Gucci. ilikuwa ni move nzuri kwa Gucci maana kwa sasa kila mtu jicho lake lipo kwa Beyonce, ame tangaza mjamzito na ana mapacha tumboni lakini pia ali slay katika Grammy’s Gucci kumtumia yeye kwa sasa it is SOMETHING ELSE

Back to our point ni kwamba, kuna wabunifu wazuri Tanzania lakini hawajui kutumia fursa like juzi katika hilo Tamasha Jokate alikuwepo akaenda kusalimiana na kina Beyonce na kila mtu alikuwa ana liongelea hilo the sad news ni kwamba Jokate alivaa nguo za adidas imagine pale ange vaa nguo kutoka kwa mbunifu wa Tanzania na mbunifu huyo ange shout kama Gucci alivyo shout.

lakini pia kuna watu kama Qboy msadi ambao wana pata fursa ya kuwavalisha wasanii wakubwa kama Diamond Platnumz lakini hawawi curious yaani kusema Diamond kavalishwa na mimi ukitaka kitu kama icho naweza kukufanyia hata usitaje bei lakini pia kuwa mbunifu mkali jaribu vitu tofauti tofauti sio kila siku tu nishirt mirefu kama mi dera.

Juzi kulikuwa na show ya LML na watu walitokelezea pale wame pendeza it was a good chance ya kuonyesha ubunifu wao kwa kuwavalisha wasanii lakini wachache sana ndio walio fanya hilo na bado pia hawaku piga makelele kuonyesha wao ndio walifanya, Jamani tembeleeni Nyota, tafuteni KIKI maana kwa sasa dunia haiendi bila hilo ila ziwe kiki zenye manufaa

wasiliana nasi kupitia

Instagram – afroswagga

Facebook – afroswaggamag

Twitter – afroswaggatz

Related posts

2 Comments

  1. important link

    … [Trackback]

    […] There you can find 99759 additional Information to that Topic: afroswagga.com/habari/jinsi-gucci-walivyo-tembelea-nyota/ […]

  2. สล็อตวอเลท

    … [Trackback]

    […] Read More Information here on that Topic: afroswagga.com/habari/jinsi-gucci-walivyo-tembelea-nyota/ […]

Leave a Reply