SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

KAMATI MPYA MISS TANZANIA
Habari

KAMATI MPYA MISS TANZANIA 

Wasi wasi ulitanda miongoni mwetu mara baada ya BASATA kuifungulia shindano la Miss Tanzania, wengi tulijiuliza kama yote yataweza kufanikishwa kwa wakati.

Kwa kutambua hilo na kuogopa yale mambo ya zamani kujirudia  Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino Agency, Hashim Lundenga leo ametambulisha mbele ya waandishi wa habari kamati mpya yenye wajumbe 12, ambayo itakuwa inaratibu mashindayo hayo kwa sasa. Ambapo wapo wadau wa urembo kama Jokate na Hoyce Temu.

Lundenga amesema kuwa kamati hiyo inayoanza kazi zake hii leo, itashughulikia mapungufu yote yaliyojitokeza na kurejesha imani ya wananchi kwa mashindano hayo ikishirikiana kwa karibu na wadau mbalimbali pamoja na Basata.

3X6A5803

Mara baada ya kutambulishwa msemaji wa kamati hiyo mpya Bi Jokate Mwegelo alikua na Haya ya kusema “Kwa niaba ya kamati mpya ya Miss Tanzania tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa uongozi wa kampuni ya Lino International Agency Limited kwa kutuamini na kututeua kuwa wajumbe wapya wa kamati ya Miss Tanzania yenye majukumu ya kuandaa, kuratibu na kusimamia mashindano ya urembo ya Miss Tanzania.

“Tumekubali na tumepokea majukumu hayo na kuahidi kusimamia kanuni, Sheria na Taratibu za kuendesha mashindano ya urembo ya Miss Tanzania.Tunaomba jamii ya Watanzania watupe ushirikiano pamoja na kutuamini kwamba tunaweza kuisogeza mbele zaidi tasnia hii ya urembo hapa nchini’

‘Kwa leo hatutakuwa na mengi ya kusema kwa sababu ndio kwanza tumekabidhiwa jukumu hili hivyo kamati yetu itakutana kupanga mipango na mikakati endelevu ya kuendeleza sanaa hii ya urembo ndani hadi nje ya mipaka yetu  ya Tanzania’ – Jokate Mwegelo

Kamati Mpya ya Miss Tanzania inaundwa na wajumbe wafuatao

1.Juma Pinto – Mwenyekiti

2.Lucas Rutta – Makamu Mwenyekiti

3.Doris Mollel – Katibu Mkuu

4.Jokate Mwegelo – Msemaji wa Kamati

5.Hoyce Temu – Mjumbe

6.Mohamed Bawazir – Mjumbe

7.Gladyz Shao – Mjumbe

8.Magdalena Munisi 0 Mjumbe

9.Shah Ramadhani – Mjumbe

10.Hamm Hashim – Mjumbe

11Khalfani Saleh – Mjumbe

12.Ojambi Masaburi – Mjumbe

Kwa upande wa Sekretariet tunao wajumbe 4 ambao ni

1.Dr.Ramesh Shah

2.Hidan Ricco

3.Yasson Mashaka

4.Deo Kapteni

Related posts

4 Comments

 1. polkadot mushroom chocolate bars review

  … [Trackback]

  […] Find More here to that Topic: afroswagga.com/habari/kamati-mpya-miss-tanzania/ […]

 2. Buy DMT online Perth

  … [Trackback]

  […] Find More to that Topic: afroswagga.com/habari/kamati-mpya-miss-tanzania/ […]

 3. Going Here

  … [Trackback]

  […] Read More Information here to that Topic: afroswagga.com/habari/kamati-mpya-miss-tanzania/ […]

 4. penis prosthetic big penis big prosthetic big dildo erect penis prosthetic

  … [Trackback]

  […] Here you will find 28680 additional Information on that Topic: afroswagga.com/habari/kamati-mpya-miss-tanzania/ […]

Leave a Reply