Kuna umuhimu wa wasanii wetu Tanzania kuwa na wabunifu, ukiacha na sauti nzuri au kuwa muigizaji mzuri lakini pia msanii hufaa kuwa na muonekano mzuri anapo kuwa kwenye maonyesho au hata pia akiwa kwenye matembezi yake ya kawaida.
Haileti picha nzuri msanii kwenda kweye red carpet hajapendeza au hata kama kapendeza basi aseme kanunua tu nguo mtaani. Ukiachana na msanii kuonekana maridadi hii pia itasaidia kukuzana kisanaa kama ambavyo msanii ata msaidia mbunifu kukua na mbunifu kumsaidia msanii.
Wabunifu wapo wengi Tanzania na wengine wadogo tu sidhani kama kuna mbunifu ambae ata weza kukataa nguo yake kuvaliwa na msanii au kumlipisha kuvaa nguo yake kwa maana msanii kuvaa nguo yako ni kukutangaza na pia msanii hupata muonekano mzuri na kuonekana ana jali muonekano wake.
Sio kitu kizuri kila mara watu kukosoa mavazi ya wasanii Fulani mara nyingi watu husema huyu hajui kuvaa, hana muonekano wa ki star, Hii hutokana na msanii kujichagulia tu mwenyewe mavazi lakini angekua na mbunifu nyuma yake hata kama angukua havai nguo aliyo ibuni huyo mbunifu basi ange mchagulia mavazi yanayo endana nae. Wenzetu nchi za nje kwa sababu wame endelea katika sekta zote mitindo na Sanaa basi wasanii hulipwa na wabunifu kuvaa nguo zao kwa sababu wana watangaza ila ilo bado hatuja lifikia Tanzania.
Wabunifu wana faa kuwafuata wasanii na kuwaomba wawavalishe pale kunapokua na onyesho Fulani ili kutangaza biashara yao. Tunaona wasanii wetu wana kosolewa au hata kufungiwa kazi zao kwa kipindi fulani kisa tu kwa kuaibishwa na mavazi yao lakini wakitoka ni yale yale yanajirudia hii ni kutokana na kukosa ushauri kutoka kwa wabunifu watu kama shilole, vanessa, linah,Ali Kiba, Linex, Ommy Dimpoz Irene uwoya , Jacqueline Wolper na wengineo wengi wamesha pata majina na wana enda sehemu mbalimbali kwa ajili ya kazi zao lakini cha kustaabisha ni nguo wazitumiazo utakuta ni za wabunifu kutoka nje. Kwanini sio Mustafa Hassan Ali? Kwanini sio Martin Kadinda? Ally Rehmtullah au Mbunifu yoyote hata kama anae chipukia? Sio tu utasababisha mbunifu akue bali pia unaweza kulitangaza vazi kutoka Africa kwamba wanaweza kukubunia Vazi kutokana na Khanga, Kitenge au hata Batiki nk.
ITAENDELEA….
UNAWEZA PIA KUTUPA MAONI YAKO
Related posts
5 Comments
Leave a Reply Cancel reply
You must be logged in to post a comment.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Here you will find 64709 additional Information on that Topic: afroswagga.com/habari/kuna-umuhimu-wa-wasanii-kuwa-na-wabunifu-wao/ […]
… [Trackback]
[…] Find More on on that Topic: afroswagga.com/habari/kuna-umuhimu-wa-wasanii-kuwa-na-wabunifu-wao/ […]
… [Trackback]
[…] Info on that Topic: afroswagga.com/habari/kuna-umuhimu-wa-wasanii-kuwa-na-wabunifu-wao/ […]
… [Trackback]
[…] Information on that Topic: afroswagga.com/habari/kuna-umuhimu-wa-wasanii-kuwa-na-wabunifu-wao/ […]
… [Trackback]
[…] Info on that Topic: afroswagga.com/habari/kuna-umuhimu-wa-wasanii-kuwa-na-wabunifu-wao/ […]