Bado tupo kwenye Swahili Fashion Week mood, na leo tunawaletea interview na mbunifu chipukizi ambaye alianza kuingia kwenye indusrty kama model Agness Nyagoha au theagness na brand yake ya Gifted Hands, haya ni machache tuliyo yapata kutoka kwake
AFRO: Waweza kutueleza kidogo kuhusu wewe, majina yako na ni lini ulianza safari hii ya ubunifu wa mavazi?
AGNESS: Naitwa Agness Nyahoga. Nilianza mwaka 2014 kama model lakini baadaye 2015 nikaamua kuwa mbunifu wa mavazi. Ubunifu wa mavazi ni kitu nilipenda toka nikiwa mdogo
AFRO: Kwanini uliamua kuhama toka kufanya modeling na kuwa mbunifu wa mavazi?
AGNESS: Nilitaka kufanya mambo makubwa zaidi kama kuvisha maraisi na watu wenye historia kubwa duniani
AFRO: Ni mara yako ya ngapi kuonesha mavazi yako katika jukwaa hili la Swahili Fashion week?
AGNESS: Ni mara yangu ya pili sasa kushiriki katika Swahili Fashion Week.
AFRO: Waionaje experience yako katika SFW? Muitikio wa watu katika kazi zako kiujumla unauonaje?
AGNESS: Imekuwa ya kipekee maana nimepokea pongezi nyingi na orders toka kwa clients, fashion producers from Kenya na South Africa pia media kwa ujumla.
AFRO: Tuzungumzie collection yako ya sasa. Inaitwaje na nini kilikuinspire kuiita hivi na the story behind it ni nini?
AGNESS: Collection hii nimeiita THE YEAR 2017. Ni kwa sababu mwaka 2017 umekuwaa mwaka wa mambo makubwa kwangu. Umenitambulisha kwa jamii pia kama mbunifu wa mavazi na brand yangu kukua. Nimeweza valisha watu maarufu nchini kama wasanii Weusi. Pia nimepokea tuzo zaidi ya moja kwa kazi hii. Hakika umekuwa wa maajabu.
AFRO: Ni fabrics na material gani zimetumika katika collection hii na ulipitia changamoto zipi hadi kuikamilisha maana ilikuwa ya kipekee?
AGNESS: Hapa ilikuwa mix ya Western na African prints. Pia ahadi kukamilika I had to think out of the box, kuwa mbunifu zaidi, kufikiria natengeneza nini na nalenga watu wa aina gani. Shopping ya materials pia, kuzunguka Karikaoo, Posta hata mitumbani. Hakika ilikuwa changamoto lakini nimeweza kujifunza mengi.
AFRO: Pia collections gani zingine zilikuvutia at the SFW?
AGNESS: (Kicheko) Dah! Kila mtu alifanya poa sana. They all had very good collections. I can say everybody deserved it kwa kweli.
AFRO: Watanzania wenye kupenda na kutaka kazi zako watakupataje? Ofisi zako na social media hadles zako ni zipi?
AGNESS: Well ofisi zangu zipo Kigogo Posta. Pia natumia @theagness on INSTAGRAM Number za simu: 0718383439
AFRO: Ushauri gani wawapa vijana majumbani wenye kupenda na kutaka kuwa wabunifu wa mavazi?
AGNESS: Waanze sasa ila wa
fanye kazi kwa viwango vya juu, hakika watafika mbali
Imeandikwa na @willibard_jr
Related posts
5 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Read More on that Topic: afroswagga.com/habari/kutana-na-the-year-2017-collection-kutoka-kwa-the-agness-sfw/ […]
… [Trackback]
[…] Find More on that Topic: afroswagga.com/habari/kutana-na-the-year-2017-collection-kutoka-kwa-the-agness-sfw/ […]
… [Trackback]
[…] Find More Information here on that Topic: afroswagga.com/habari/kutana-na-the-year-2017-collection-kutoka-kwa-the-agness-sfw/ […]
… [Trackback]
[…] There you can find 42186 more Info to that Topic: afroswagga.com/habari/kutana-na-the-year-2017-collection-kutoka-kwa-the-agness-sfw/ […]
… [Trackback]
[…] Read More Information here on that Topic: afroswagga.com/habari/kutana-na-the-year-2017-collection-kutoka-kwa-the-agness-sfw/ […]