SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

KUTOKA KWETU KWENDA KWA LINDA BEZUIDENHOUT NA MANGE KIMAMBI
Habari

KUTOKA KWETU KWENDA KWA LINDA BEZUIDENHOUT NA MANGE KIMAMBI 

Mange Kimambi na Linda Bezuidenhout ni wabunifu kutoka Tanzania ambao wote kwa sasa wana ishi na kufanya kazi zao Nje ya Nchi. Ilikua mategemeo yetu kwa wawili hawa kuiletea sifa Nchi yetu si kwa mafanikio ya mmoja mmoja bali ya wote wawili, tukimaanisha wafanye kazi kwa kushirikiana ili kupata matokeo mazuri Zaidi, waswahili husema “umoja ni nguvu na utengano ni idhaifu” na hivyo ni namna ya Watanzania wengi waishio nje na ndani ya Nchi tunavyo ishi.

index

Lakini tofauti na mategemeo ya wengi wawili hawa wamekua wakitukanana mitandaoni na kuleta picha mbaya, hii ina fanya kuleta utengeno kati ya mashabiki ambao pia ni wanunuzi wa bidhaa zao iwe ndani au nje ya Nchi, ni kweli hawa wawili wote wana vipaji vya kubuni kama ukiangalia kazi ya Linda au Mange lazima utavutiwa nayo lakini wawili ni wawili ina wezekana wakishirikiana wana weza kutoa kitu kizuri na kilicho bora Zaidi.

Wawili hawa wana takiwa kufuta tofauti zao ili kuweza kuitangaza Nchi yetu vizuri kwa mavazi yetu na kutangaza ubunifu wetu katika Nchi wanazo ishi, haipendezi kuona wa-Tanzania waliopo nje ya Nchi wana shindwa hata kuombana chumvi. Tunaamini Mange na Linda wote wana pigania kilicho bora kwa ajili ya Tanzania na kama wakishikana basi watakua na nguvu tosha ya kuweza kufanikisha malengo yao.

Related posts

2 Comments

  1. Best Psychedelic Store Melbourne

    … [Trackback]

    […] There you can find 49175 additional Info to that Topic: afroswagga.com/habari/kutoka-kwetu-kwenda-kwa-linda-bezuidenhout-na-mange-kimambi/ […]

  2. บ้านมือสอง

    … [Trackback]

    […] Find More on that Topic: afroswagga.com/habari/kutoka-kwetu-kwenda-kwa-linda-bezuidenhout-na-mange-kimambi/ […]

Leave a Reply