Kwa wale wafuatiliaji wa mitindo mtajua katika Nchi za wenzetu kuna seasonal collections ( matamasha ya fashion ya kila msimu), Nigeria wamemaliza Nigeria Fashion Week ambayo hii ilikuwa ni Autumn & Winter Fashion Week lakini pia tunaona South Africa wanaanza South Africa Fashion Week ambayo hii ni ya SS18 yaani Spring/Summer 2018, kwa wale ambao mtakua mnajiuliza Afroswagga wanaongelea nini? Tunaposema fashion week za msimu tunamaanisha misimu ya mwaka yaani majira ya mvua, kiangazi, baridi na kipupwe
Haya ni majira ya mwaka huwa yanatokea kila baada ya miezi fulani kama sasa hivi tupo katika majira ya mvua, mvua zinanyesha mara kwa mara na baridi. Huko kwa wenzetu kila ambapo msimu unaisha na mwingine kuanza wana matamasha ya mitindo ambayo wana introduce au ku debut collection zao mpya ambazo zinaendana na msimu huo. Lakini cha kushangaza hapa kwetu hakuna kabisa system hio matamasha yetu makubwa ni mawili ambayo ni Red In Lady Fashion Show na Swahili Fashion Week ambayo mtu ana debut collection yake moja ya mwaka mzima kama ataamua kuwavalisha models nguo za masika basi ndio hiohio itakua ya mwaka mzima, kama za kiangazi basi ndio hizohizo.
Wabunifu wengi wanaenda na kisingizio cha misimu haileweki au kwamba Tanzania hatuna baridi kiasi hicho mpaka tuwe na collection za msimu wa baridi peke yake, joto peke yake n.k, lakini hapo hapo Nchi nyingi za Africa pia misimu yake kama yetu hamna baridi hadi barafu lakini wao wana aina hii ya matamasha. Je ni kwanini sisi hatuna?
Kwanini tumeuliza hili swali
Aina hii ya matamasha itasadia kukuza majina ya wabunifu na sio ku debut collection moja halafu watu hawakusikii tena mpaka mwakani na sio kwa wabunifu tu hii ni hata kwa wanamitindo (models) itasaidia wao kupata kazi mara kwa mara na kulizoea jukwaa.
Lakini pia kuimarisha ubongo wa mbunifu, hapa wabunifu watajitaidi kufikiria kubuni kutokana na majira, kujua nini kinaendelea Duniani. Vazi lipi ni la msimu upi kwa sasa wanatoa colletion moja na utakuta ni ya kawaida mno unapokuwa una toa collection nne kwa mwaka hapo ndipo watajitaidi kuumiza vichwa vya kipi kinafaa msimu upi, msimu huu nini kina trend lakini pia kujitahidi kubuni vitu vya tofauti zaidi ili kuonekana wa tofauti.
Itawezesha watu kupenda vya kwetu linapo kuja swala la kununua mavazi ya kwetu wenyewe inakuwa mtihani hasa pale kama kuna kipindi cha baridi halafu mbunifu wako collection yake ni ya msimu wa kiangazi, inakulazimu uangalie wabunifu wengine wa nchi nyingine ili kupata unacho hitaji mwishoe misimu yote mitatu tunanunua kwa wabunifu wa nje wakati msimu mmoja tu ndio tunanunua vya kwetu. Hii itasaidia mzunguko wa pesa kuwa hapahapa na sio kutoa Nje.
Well kwa wale ambao mngependa tuwe na collection zote za misimu hii minne tupaze sauti ili wahusika wasikie na tuanze kupata tunacho kihitaji.
Related posts
5 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Info to that Topic: afroswagga.com/habari/kwanini-tanzania-hatuna-matamasha-ya-mitindo-kwa-kila-msimu/ […]
… [Trackback]
[…] Read More on that Topic: afroswagga.com/habari/kwanini-tanzania-hatuna-matamasha-ya-mitindo-kwa-kila-msimu/ […]
… [Trackback]
[…] Read More on to that Topic: afroswagga.com/habari/kwanini-tanzania-hatuna-matamasha-ya-mitindo-kwa-kila-msimu/ […]
… [Trackback]
[…] Find More Info here to that Topic: afroswagga.com/habari/kwanini-tanzania-hatuna-matamasha-ya-mitindo-kwa-kila-msimu/ […]
… [Trackback]
[…] Read More Information here to that Topic: afroswagga.com/habari/kwanini-tanzania-hatuna-matamasha-ya-mitindo-kwa-kila-msimu/ […]