- Mustafa Hassanali amealikwa katika hekalu la Buckingham
- Kampuni ya Rwanda Air kumsafirisha Mustafa Hassanali kuelekea uingereza.
- Nguli wa mitindo barani Afrika, Mustafa Hassanali amealikwa katika shughuli ya kubadilishana mawazo kuhusu mitindo kwa nchi za jumuiya ya madola.
Nguli wa mitindo barani Afrika ambaye ametunukiwa tuzo mbalimbali, Mustafa Hassanali, ameweza kukamata jicho la familia ya kifalme, Nguli huyo wa mitindo atakuwa mgeni moja wapo kati ya wabunifu wengine wa kimataifa kutoka nchi mbalimbali za jumuiya ya madola, watakaoshiriki katika shughuli ya kifahari kuhusu mitindo, katika hekalu la malikia wa Uingereza huku wakisherekea ubora wa kazi za ubunifu.
Mustafa Hassanali amepokea mwaliko ambao haukutarajiwa unaomtaka kushiriki katika sherehe ya kubadilishana mawazo kuhusu mitindo kwa nchi za jumuiya ya madola itakayofanyika katika hekalu la Buckingham tarehe 19 mwezi huu, mbele ya uwepo wa Catherine Elizabeth Mountbatten-Windsor (Kate Middleton) na Sophie Countess of Wessex amabo ni mabint kutoka familia ya kifalme
“Ni heshima kubwa na ufahari kualikwa katika sherehe hii ya kifahari ikayofanyika katika hekalu la Buckingham kwa amri ya Malikia na kuweza kusherekea nae kazi za mitindo kutoka nchi zote za jumuiya ya madola, hii inaonyesha kuwa kazi yako na kujitolea katika sekta ya mitindo ya Tanzania inakubaliwa na kutambuliwa kimataifa.” Alisema Mustafa Hassanali.
Aliongeza kuwa “ Nashukuru kwamba , kwa miaka mingi nimeleta mabadiliko mabayo nilitamani kuyaona katika sekta ya mitindo ya hapa nchini, kama Rais wa Marekani Marehemu John F Kennedy alivyosema, usiulize nini nchi yako inaweza kukufanyia, jiulize nini unaweza kufanya kwa nchi yako.kwa miaka kumi iliyopita nilianzisha na kuandaa jukwaa kubwa la mitindo Afrika Mashariki na Kati lijulikanalo kama Swahili Fashion Week, na hivi karibuni ni nimekuwa mwanachama mwanzilishi na mwenyekiti wa Kampuni ya kukuza kazi za mitindo na ubunifu hapa nchini (Fashion Association of Tanzania) ambacho kina nia ya kujenga na kuimarisha vipaji na sekta ya mtindo ya Tanzania.
Mchango wa Mustafa Hassanali katika sekta ya mitindo nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla haujaenda bure, shirika la ndege ya kitaifa ya Rwanda, imewezesha safari ya Mustafa iliapate uzoefu wa ndoto ya kusafiri kutoka Afrika hadi mji wa Gatwick nchini Uingereza kupitia ndege yao ya mfululizo wa A330-300.
“Ni heshima kubwa na tunajivunia kuweza kumsafirisha nguli wa mitindo Mustafa Hassanali aweze kuhudhuria sherehe ya mitindo iliyoandaliwa kwa nchi za jumuiya ya madola itakayofanyika katika hekalu la Buckingham. Vilevile ndege zetu zinasafilisha mara mbili kwa siku kutoka Dar es Salaam hadi Kigali na miji mingine 23 kutoka Kigali na nchi nyingine zaidi” alisema Meneja wa Rwanda Air nchini Tanzania, Bw.Ibrahim Bukenya.
Sherehe hiyo ya kubadilishana mawazo kuhusu mitindo kwa nchi za jumuiya ya madola, zitakuwa na wabunifu 52 na wataalamu wa sanaa za mikono kutoka nchi tofauti za jumuiya ya madola, wataungana kutengeneza nguo moja ya kipekee na endelevu, ambayo itaonyeshwa katika sherehe hiyo itakayofanyika katika hekalu la Buckingham, huku nguo hiyo ikiwa na lengo kutumia jumuiya ya madola pamoja na nafasi ya biashara ya mitindo ya wataalamu wa sanaa za mikono inaweza kuleta matokeo chanya katika kuwawezesha wanawake na kupunguza umasikini.
Related posts
2 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Find More on to that Topic: afroswagga.com/habari/malkia-wa-uingereza-amualika-mbunifu-mustafa-hassanali-katika-commonwealth-fashion-exchange/ […]
… [Trackback]
[…] Find More Information here to that Topic: afroswagga.com/habari/malkia-wa-uingereza-amualika-mbunifu-mustafa-hassanali-katika-commonwealth-fashion-exchange/ […]