Aliye kuwa Miss Tanzania Hapiness Magesse jana ame introduce logo ya kampuni yake pamoja na kumu introduce ata kae iwakilisha Tanzania katika Miss Africa 2016, ambapo mashindano haya yame anzishwa mwaka huu na yata fanyika Nigeria Jimbo la Cross River mji wa Calabar tarehe 26 November mwaka huu
Mrembo Julitha Kabete ame pata nafasi ya kutuwakilisha katika mashindano hayo, Julitha ame shiriki Miss Tanzania mwaka huu
Julitha aliandika haya katika ukurasa wake wa Instagram
Naitwa Julitha Kabete. Ni mrembo ambaye nitawakilisha Tanzania katika mashindano ya urembo ya kufatuta mrembo wa Afrika 2016. Mashindano haya yatafanyika nchini Nigeria, jimbo la Cross River state mjini Calabar tarehe 26, novemba 2016. Miss Africa 2016, imeanzishwa mwaka huu, kwahiyo haya ni mashindano ya kwanza. Mashindano haya ya Miss Africa 2016 yamebeba kauli mbiu “green economy, a tool for sustainable development” yaani Uchumi unaozingatia, kutunza n.a. kujali mazingira. Kwahiyo mashindano ya Miss Africa 2016 yanatafuta mrembo ambaye atatangaza na kuwakilisha utunzaji wa mazingira na maendeleo endelevu. Nitahamasisha na kusaidia wananchi kuelewa madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi ( climate change). Pia nitaitangaza Nchi yangu ya Tanzania nje ya Nchi n.a. kimataifa na kuungana na taasisi mbalimbali kusaidia na kutafuta suluhisho na kupunguza madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi. Mfano wa mabadiliko ya tabia nchi ambayo yanaleta wasiwasi sana ni kama tatizo la mlima wa kilimanjaro. Mlima unaotupa sifa za kila aina duniani na watu kuona uzuri wa nchi yetu. Kwa sasa mlima wetu upo hatarini na Kupoteza hadhi yake kutokana na barafu iliyopo katika mlima huo kuanza kuyeyuka kwa kasi ya ajabu ambayo imesababishwa na mabadiliko ya tabia nchi. Utafiti wa wanasayansi unaonyesha kuwa kama Hali itaendelea kuwa hivi, barafu katika mlima kilimajaro inaweza kutoweka kabisa ifikapo mwaka 2025. Huu ni mfano unao onyesha jinsi mabadiliko ya tabia nchi yanaweza kutuharibia mazingira na pia kutokua kiuchumi. Kuna mengi ambayo yanatukumba watanzania kutokana na mabadiliko ya tabia nchi. Huo mfano ni moja ya swala ambao nitaongelea sana nikiwa Nigeria. Kwahiyo, naenda kuwakilisha nchi yangu hasa kwenye suala zima la mabadiliko ya tabia nchi yanayosababishwa na vitu mbalimbali kama ukataji miti ovyo na uvuvi usio wa kitalaamu unaotukumba. Nimefurahi kwamba watanzania mwaka huu tumesisitiza na kutekeleza sana upandaji wa miti. #mtiwangu Nawahaidi kuwa balozi mzuri kwenye hili swala. Na nita post kila siku kujulisha events zinazoendelea Miss Africa 2016. Naomba tushirikiane sababu ninaenda kubeba na kuitangaza nchi.
Wakati Millen yeye alia ndege wawili kwa jiwe moja kwa ku-introduce kampuni yake pia kumu introduce Julitha
Kampuni tanzu za MMG (Millen Magese Group of Companies) ina furaha kubwa kupewa heshima na fursa ya kutuma Mshiriki kutoka Tanzania kama mwakilishi wa Taifa katika mashindano ya kipekee na ya aina yake yanayojulikana kama Miss Africa 2016 yatakayofanyika katika jimbo la Cross River huko Calabar nchini Nigeria tarehe 26.11.2016. Tunatoa pongezi kubwa kwa Mwakilishi kutoka Tanzania Julitha Kabete (19) na kumtakia kila la kheri tukiwa na matumaini makubwa ya yeye kuliletea Taifa ushindi kama Balozi na Muwakilishi. Mashindano haya yamebeba ujumbe wa Maendeleo ya Kiuchumi yanathamini, kujali na kutunza Mazingira . Tunatoa shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa n.a. Michezo Mh.Nape Moses Nnauye, Wazazi wa Julitha Kabete, Kamati nzima ya Miss Tanzania (iliyomvumbua Binti huyu), Wanahabari wote na kila Mtanzania . MMG inatoa wito kwa wa watanzania wote kumpa ari , hamasa na ushirkiano wa kutosha mwakilishi wetu katika mashindano haya ya Miss Africa 2016 (www.miss africa.tv) Kama ambavyo imekuwa ikifanya kwa miaka takribani sita sasa tangu kuanzishwa kwake kuendeleza na kuvitambulisha vipaji vya Tanzania kwa Afrika na Dunia. MMG itaendelea na kujikita zaidi kuona vijana wengi zaidi wanapata fursa za kuweza kuitangaza nchi yetu vyema kimataifa na kuweza kupata fursa kuwa mifano bora na kusaidia wengine zaidi. Asanteni sana na tungependa pia kumpongeza na kumtakia kila la kheri Binti mwingine ambae ni Mshindi wa Miss Tanzania 2016 Diana Lukumai, maadalizi mema kupelekea kuiwakilisha Nchi katika mashindano ya Dunia. Kila la kheri Tanzania. Millen Magese 🙏Cc @mmgcoltd
Related posts
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…