kama ni mfuatiliaji wa mambo ya urembo basi utakuwa una kumbuka hili, Miss Tanzania ilipata sekeseke la kufungiwa kwa takribani mwaka mmoja kutokana na kutokea mtafaruku katika shindano hilo, mpaka pale shindano lilipo funguliwa tena katikati ya mwaka huu ambapo walitakiwa kufanya mabadiliko katika management na mambo mengine madog madogo, kweli ilifanyika na shindano likaanza ma miss wakaanza kutafutwa kuanzia vitongojini mpaka juzi jumamosi ambapo tulipata kumpata muwakilishi wetu mpya katika Miss World.
Lakini ina onekana bado kuna tafrani as watu hawaja mpokea vizuri miss huyu mpya kuna mambo mbali mbali yanaendelea huko mitandaoni ikiwemo na kusema kwamba miss kadanganya miaka na matokeo yake ya kidato cha nne
Japo mwenyewe ame jibu tuhuma hizi kwa kuanduka yafuatayo katika ukurasa wake wa Instagram.
TAARIFA KWA UMMA Napenda kuujulisha Umma yafuatayo; 1. Miss Tanzania 2016/2017 aliyeshinda taji jana jijini Mwanza, anaitwa Diana Edward Loy na siyo Diana Lukumai kama inavyotajwa mitandaoni. 2. Mlimbwende huyo amemaliza kidato cha nne 2015 Shule ya Sekondari Arusha Day na si 2011 kama inavyotajwa mitandaoni kwa malengo ovu. 3. Diana hajawahi kujiunga na Elimu ya Chuo Kikuu chochote Tanzania au duniani bali anatarajia kujiunga mwaka huu katika chuo cha IFM kusomea masula ya kodi ngazi ya stashahada (cheti) ingawa kulingana na ratiba zake na majukumu yake mapya ikiwemo kushiriki Miss world mapya huenda akaahirisha mwaka wake wa masomo. 4. Tunawasihi watanzania kutumia vyema mitandao ya kijamii na si kufanya “Character assassination” lakini pia tunaheshimu haki yao ya msingi ya kuhoji masuala ya msingi kabisa kuhusu mtu ambaye ni Public figure na ataliwakilisha taifa katika anga za kimataifa. Tumuunge mkono mlimbwende wetu ili atuletee Taji la Dunia. Ahsanteni. Charles William Kaimu Ofisa Habari wake. 0716719589 (wilflow101@gmail.com). CnP @RepostIt_app
Diana Binti wa kimasai mwenye miaka 18 ame twaa taji la urembo wa Miss Tanzania 2016 akifuatiwa na Grace Malikita na Maria Peter
Baadhi ya wadau wa urembo wana sema bado sekta ya Miss Tanzania haija jiandaa vizuri katika uandaaji wa shindano hili kwamba sherehe haikuwa nzuri ni kama ana tafutwa miss kitongoji
Swali ni moja je we will stand a chance kushinda miss world? ikumbukwe tuna peleka mshiriki ambae ataenda ku compete na warembo mbali mbali duniani, nadhani we still have a long way to go kama tuna taka kushinda Diana ana takiwa anze kujiandaa kuanzia sasa unless kama tuna kubaliana na matokeo ya kwenda kushiriki na kurudi bila taji kila mwaka.
Related posts
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…