SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

MISS TANZANIA DIANA ASEMA HANA MAANDALIZI YA MISS WORLD
Habari

MISS TANZANIA DIANA ASEMA HANA MAANDALIZI YA MISS WORLD 

Ikiwa ni siku chache tu toka atwae taji la Miss Tanzania Mwanadada Diana ameanza kulalamikia uongozi wa Miss Tanzania kwamba kuna mengi yana hitaji kufanyika na hapewi support ya uhakika, hili lime kua tatizo kwa miaka nenda rudi nadhani ni wakati wa waandaji wa shindano hili kubadilika.

Diana alikuwa na haya ya kusema wakati akihojiwa katika kipindi cha planet bongo east africa radio

DSC_0406

“Hata zawadi zangu zilizo haidiwa sijapewa, kwahiyo inakuwa ngumu kwangu kujiandaa na mashindano ya miss dunia,” Diana alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio. “Siku ishirini zilizobaki ni ndogo natakiwa kuandaa documentary ya historia ya kimasai Arusha. Sina kitu chochote chakufanyia natakiwa nilipe hiyo, natakiwa nilipe team support kwa sababu natakiwa kwenda kuonyesha Tanzania yangu, natakiwa kuonyesha beauty of purpose,”

Aliongeza, “Tanzania, viongozi, serikai, Miss Tanzania cometee, i need suport, i need what i deserve, unajua mimi ni mtu ambaye najiongeza, kwa hiyo nikipewa suport kidogo i push it up, kuna watu ambao nimewaomba suport wamenipa vya kutosha, kwa hiyo i need what i deserve”

Kwa upande wa afisa uhusiano wa kamati ya Miss Tanzania, Hidan Rico amesema shughuli za maandalizi ya miss huyo zinafanywa na Kamati ya Miss Tanzania.

“Hayo mambo yanashughulikuwa na Kamati ya Miss Tanzania. Yaani ameshaanza kuongea na vyombo vya habari? Mimi sina mamlaka ya kulijibu hilo la zawadi lakini nachojua maandalizi yake yanafanyika na kamati,” alisema Rico.

tupe moani yako kupitia

Instagram – afroswagga

Facebook – afroswaggamag

Twitter – afroswaggatz

Related posts