SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

MISS UTURUKI HATIANI KWA KUMTUKANA RAIS
Habari

MISS UTURUKI HATIANI KWA KUMTUKANA RAIS 

Huko Uturuki habarikubwa ni hii ya Mahakama kwenye mji wa Istanbul kumhukumu mshindi wa zamani wa shindano la urembo nchini Uturuki kwa kosa la kumtukana rais wa nchi hiyo Recep Tayyip Erdogan.

recep-tayyip-erdogan

Kwa mujibu wa BBC Swahili , Merve Buyuksarac mwenye umri wa miaka 27 alipatikana na hatia ya kumtukana hadharani President wa Uturuki hivyo amehukumiwa kifungo kilichoahirishwa cha miezi 14 gerezani.

missturkey

Inasemekana pia mrembo huyu aliandika kwenye mtandao wake wa kijamii pamoja na kuwatumia watu shairi lenye matusi katika mtandao wake wa Instagram lakini Wakili wake amesema wamepinga hukumu hiyo katika Mahakama kuu ya bara la Ulaya na Buyuksarac amekanusha madai yote dhidi yake.

 

Wanaharakati wa kupigania haki za Binadamu wanasema hiyo kesi ni njia ya serikali ya rais Erdogan kukandamiza uhuru wa kujieleza ambapo hadi sasa watu 2000 wengi wao wakiwa ni Wasanii nyota na hata wanafunzi wameshtakiwa kwa kumkejeli au hata kumtusi Rais huyu tangu mwaka wa 2014.

BBC wameripoti kwamba hukumu hiyo iliahirishwa ilimradi tu asirudie makosa hayo katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Related posts

2 Comments

  1. Drostanolone Enanthate Kaufen

    … [Trackback]

    […] Find More on that Topic: afroswagga.com/habari/miss-uturuki-hatiani-kwa-kumtukana-rais/ […]

  2. hk usa

    … [Trackback]

    […] Find More on that Topic: afroswagga.com/habari/miss-uturuki-hatiani-kwa-kumtukana-rais/ […]

Leave a Reply