Witnes, Tiffa Flow, Nician, Stosh, Chiku Keto, Chemical, na, hawa ni wachache kati ya wengi wanaofanya muziki wa kizazi kipya katika upande wa hiphop. Lakini kabla ya hawa kulikuwa na wasanii kama Zay B, Sister P, pamoja na Raha P
Moja ya maswali ambayo wakati wote hujiuliza ni juu ya muonekano wao, wengi wao kama sio wote hupenda kuvaa mavazi ya kiume. Siachi kujiuliza je wanadhani ukiimba hiphop ni lazima uvae mavazi hayo ya kiume tena suruali au pensi chini ya makalio?
Stosh Tz female rapper
Hakika muonekano wao hufanya mashabiki na wadau waone kama ni watu wahuni tu maana iko wazi mtoto wa kike sharti upendeze wakati wote. Ila wasanii hawa wa kike mara zote huwakuta wakiwa na muonekano ambao haipaswi msanii kuwa hivyo.
Ila katika wasanii wa kike ni msanii mmoja tu mwenye muonekano mzuri na kistaa ambaye ni Tammy The Baddest
Lakini kwanini hawaigi mfano Tammy The Baddest au hata wa Nick Minaj na Iggy Azalea? Maana hawa ni wasanii wa hiphop na wameweza kuchukua tuzo nyingi na kubwa duniani ila muonekano wao ni mzuri yani vile inavyopaswa mtoto wa kike aonekane. Tatizo ni nini kwa wasanii wetu?
Inashangaza leo hata katika mahojiano ni kawaida kabisa kwa msanii husika kwenda katika mahojiano akiwa katika muonekano mbaya kuanzia mavazi mpaka aina ya nywele au jinsi alivyonyoa. Chemical ni mfano tosha, juzi hapa akiwa anatambulisa wimbo wake.
Nguo alizovaa jinsi alivyoweka nywele ni wazi hakuwa na muonekano mzuri, ni vyema kuamka kifikra wasanii hawa wa kike kwenye muziki wa hiphop wajue wanaweza kupendeza na kufanya vyema kwenye muziki huo.
chemical Tanzania female rapper
Related posts
6 Comments
Leave a Reply Cancel reply
You must be logged in to post a comment.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Find More Info here on that Topic: afroswagga.com/habari/muonekano-una-wafelisha-female-rappers-wa-tanzania/ […]
… [Trackback]
[…] Info on that Topic: afroswagga.com/habari/muonekano-una-wafelisha-female-rappers-wa-tanzania/ […]
… [Trackback]
[…] There you can find 97671 more Info on that Topic: afroswagga.com/habari/muonekano-una-wafelisha-female-rappers-wa-tanzania/ […]
… [Trackback]
[…] Find More to that Topic: afroswagga.com/habari/muonekano-una-wafelisha-female-rappers-wa-tanzania/ […]
… [Trackback]
[…] Read More Information here on that Topic: afroswagga.com/habari/muonekano-una-wafelisha-female-rappers-wa-tanzania/ […]
… [Trackback]
[…] There you will find 48939 additional Info on that Topic: afroswagga.com/habari/muonekano-una-wafelisha-female-rappers-wa-tanzania/ […]