SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Namna Mbalimbali Za Kuvaa Nguo Za Leather
Habari

Namna Mbalimbali Za Kuvaa Nguo Za Leather 

Moja kati ya material ambayo fashionista wengi hutumia katika mavazi yao ku-stand out (kuwa watofauti) ni material ya leather. Si watu wengi ambao sio fashionista’s wanamiliki mavazi ya material haya, lakini ni material ambayo ni nzuri inayokufanya uonekane wa tofauti na kama utachagua material nzuri basi inakupa rich feeling.

Well katika pitapita zetu tumegundua kwa sasa fashionistas wengi wanatumia material hii kwa lugha nyingine tunaweza kusema ina trend, from Rihanna, Vanessa Mdee, Mwamvita Makamba, Julitha Kabete na wengine wengi wakiwa ndani ya trend hii.

Tunaweza kuwaona Julitha Kabete Na Mwamvita Makamba walivyo suruali zao za leather. Badala ya kuvaa suruali za jeans au kitambaa kama ambavyo wengi tumezoea wao walichagua ku-stand out kwa kuvaa suruali za leather na kama ambavyo mnaona they look chic & stylish.

Namna nyingine ambayo ina trend sana kwa sasa ni leather skirts, kama ambavyo tunawaona Mary Claverys na Kefilwe Mabote wakiwa wamevaa za kwao, Mary yeye alichagua kuvaa Min skirt nyeusi, akamaliza na graphic tee pamoja na yellow min bag na white strap sandals. Wakati Kefilwe yeye alichagua kuwa bold kwa kuvaa red leather skirt, t shirt nyeupe, akamalizia na handbag ya kijani, metallic pumps na miwani.

Unaweza kuchagua kuvaa two pieces kama Rihanna au Vanessa Mdee na bado ikanoga, kitu ambacho tumeona wote wako nacho sawa ni kwamba wakivaa leather hawaweki mambo mengi, yaani they let the leather do the talking.

Khanya Mkangisa Looks Sexy in her short black leather dress.

Lakini pia unaweza kuvaa kama Jumpsuit kama ambavyo Flaviana Matata Amevaa

Related posts

1 Comment

  1. เฟอร์นิเจอร์สำนักงาน

    … [Trackback]

    […] Find More to that Topic: afroswagga.com/habari/namna-mbalimbali-za-kuvaa-nguo-za-leather/ […]

Comments are closed.