Katika Kuendeleza shauku ya kutafuta kizazi kipya cha wabunifu wa mavazi, Maonyesho makubwa ya mavazi nchi tanzania yanakuletea mashindano ya kumtafuta wabunifu chipukizi na kuwapa nafasi wataokao staili kuweza kujulikana kitaifa na wanunuzi wa bidhaa ili kuweza kuwaunganisha na fursa za soko la tasnia ya mitindo ili kupata msaada wa kukuu na kupata faida..
“wabunifu chipukizi ni tasnia ya mitindo ya miaka ijayo, na mashindano yetu ni sehemu ya jukwaa kwa ajiri ya vipaji vya ajabu ambavyo havijajulikana na kuwaonganisha na watu waliopo katika tasnia ya mitindo ambao wanatafuta mbunifu mkubwa wa baadae,sheria za shindano hili katika swahili fashion week kuna nafasi za wabunifu nane tu kati ya wengi watakaoomba, kutokana na maombi kuwa mengi mpakasiku ya mwisho ya tumepokea maobi zaidi ya mia moja , tumeamua kuongeza nafasi mbili kutokana na kazi zao kuwa nzuri na ustadi wa hali ya juu, hivyo, baadaya uchaguzi wa majaji ni washindani kumi tu ambao wataingia katika shindano hili. Alisema mratibu wa mitindo, wa maonyesho ya swahili fahsion week Bi Lightness Kitua.
Katika kipindi cha miaka saba iliyopita, tangu mwaka 2008 Swahili Fashion Week walipoanza kutafuta wabunifu chipukizi, wamekusanyika zaidi ya wabunifu 800 wenye vipaji kutoka Afrika ambao wanaendelea kufanya ubunifu wa mavazi endelevu, kwa kuonyesha nguo zao katika majukwaa mbalimbali makubwa duniani ambao walizindua kazi zao katika jukwaa la swhaili fshion week, badhi ya wabunifu hao ni Martin Kadinda, Sara Mmasenga, Subira Waule, Kiara Sheba, Mtani Nyamakababi na wengine wengi.
“tunashuhudia matunda ya washindi waliopita katika mashindano haya ya kutafuta mbunifu chipukizi,ambao wamebadilisha tasnia ya mitindo na kuwa dunia nzuri ya mitindo, mwaka huu tunatafuta mbunifu mwenye kipaji ambaye yupo wazi kwaajiri ya biashara na mwenye shauku ya mafanikio, na tutaendelea kukuza kazi yake katika mitindo endelevu, kwa njia ya kumuunganisha na wabunifu wakubwa , kumtangazia biashara yake na kukuza uelewa wake katika ubunifu hili aweze kufanikiwa katika soko la mitindo” alisema lightness
“Mwaka huu washindani walichukua mandhari ya nguo vizuri sana. Michoro yao ya mavazi ni mizuri na ya asili, kwaiyo ikawa ngumu kuchagua washindani kumi watakaobaki. Ninasubiri kuona ubunifu wao wa mwisho katika jukwaa la Swahili Fashion Week , kama watakuwa na uwezo wa kuonyesha ambacho wameweza kuonyesha awali katika kufata mandhari ya mwaka huu ya kumuenzi marehemu Washington Benbella ambaye alikuwa meneja miradi wa Swahili Fashion Week.
Jina kubwa la mshindi wa mbunifu chipukizi wa Swahili Fashion Week atapata nafasi au fursa ya kuonyesha nguo zake za ubunifu katika jukwaa la Swahili fashion week, nguo hizo zikipita mbele ya watazamaji ambao ni wadau wa mitindo kutoka Tanzania na nchi zingine duniani.
Mchakato huo uliongozwa na jopo la majaji ambao ni wabunifu na wadau wa mitindokama Jamilla Vera Swai, Noel Ndale, Hamis Omary, Na lightnes Kitua Mratibu wa Swahili Fashion Weeek, majaji hao walichangua vipaji 10 vya awali ambao ni Shahbaaz Sayed, Andrew Kalema, Ruth Chimbala, Anna Peter, Elizabeth Alphonce, Nadeem Ibrahim, Anna Paul, Agness Nyahoga, Sharmila Ibrahim, na Justina Thomas. mchakato utaendelea mpaka kupatikana mshindi mmoja tu amabay atatangazwa siku ya mwisho ya maonyesho haya yatakayo fanyika katika Makumbusho ya Taifa kuanzia tarehe 02- hadi 04 disemba mwaka huu.
MWISHO
MEDIA INQUIRES
maryam@361tanzania.com
Related posts
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…