SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Ongezeka La Ushuru Kwenye Nywele Bandia Na Mavazi Ya Mtumba
Habari

Ongezeka La Ushuru Kwenye Nywele Bandia Na Mavazi Ya Mtumba 

Bajeti ya serikali kwa mwaka 2019/2020 imesomwa jana Bungeni na Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Philip Mpango. Kimsingi ni bajeti ambayo umelenga kuondoa mzigo kwa mwananchi wa kawaida na kuongeza thamani ya mazao na bidhaa zinazozalishwa nchini. Bajeti yote kwa ujumla imelenga sekta zote za uchumi  na uzalishaji. Lakini tutagusia maeneo  machache ambayo yamegusa sekta yetu ya ubunifu wa mavazi na urembo.

  • Kuongezeka kwa ushuru wa mtumba kwa 35%

Sote tunatambua kuwa mavazi ni hitaji la msingi kwa mwanadamu, na wengi wetu tumeekuwa wavaaji wa kubwa wa mitumba kutoka nje ya nchi. Lakini kupitia bajeti hii serikali imeongeza ushuru kwenye mitumba itokayo nje ya nchi. Ongezeko lolote la kodi au ushuru huwa ni mzigo wa mnunuzi wa mwisho (mtumiaji). Lakini hatua hii inatija kwa wazalishaji wetu waliopo kwenye mnyororo wa thamani kuanzia kwa mkulima mpaka kwa mshonaji. Tunapenda kuipongeza serikali kwa uamuzi huu kwa sababu utaleta chachu kwa wazalishaji wa ndani na kuongeza nyororo wa thamani kutoka kwa mbunifu ambaye atachora na mkulima atakayeuza pamba yake kwa mwenye kiwanda, mwenye kiwanda atazalisha vitambaa mbalimbali na nyuzi, mbunifu atabuni vazi ambalo atampa fundi aishone. Hatimaye kumfikia mvaaji ambaye atavaa kitu kikiwa kipya na kwa bei nafuu. Nadhani sasa ni wakati wa wabunifu wetu kuchangamikia fursa na kuanza kubuni aina nyingi zaidi ya nguo kwa kuwa soko litaongezeka.

 

  • Ushuru wa nywele bandia

 

Bajeti hii imegusa pia sekta ya urembo hususani wa wanawake, wale ambao tunapendelea kuvaa nywele bandia. Katika bajeti hii nywele bandia zimeongezwa ushuru wa asilimia 10% kwa zinazotengenezwa na makampuni ya ndani na ongezeko la asilimia 25% kwa nywele bandia zinazoingia kutoka nje ya nchi. Kuweka tofauti ya ushuru kati ya nywele za ndani na zile za nje ni mkakati ambao serikali imelenga katika kuvutia uwekezaji wa viwanda vya nywele na kuhamasisha masoko ya ndani ya nywele zinazotengenezwa ndani. Hili pia ni la kupongezwa kwasababu uzalishaji utaongezeka kwa kuwa watumiaji wa nywele za zinazozalishwa ndani wataongezekwa kuwa zitakuwa nafuu ukilinganisha na zile zinazozalishwa nje. Uzalishaji ukiongezeka, viwanda vitahitaji malighafi pamoja na nguvu kazi hapo ndipo akina sie tunapata kazi, vyuma vinalainika. Tukipata kazi tutapata pesa ambayo itatufanya tumudu kununua hata hizo nywele na kujipamba ziadi.

Related posts