SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Our Two Cents On Yanga Outfit’s At White House Dinner
Habari

Our Two Cents On Yanga Outfit’s At White House Dinner 

Kwanza kabisa tuanze na hongera kwa Yanga kwa kututoa kimasomaso baada ya miaka mingi kupita, kama Nchi tuko proud na hii achievement.

Turudi kwenye vazi la Yanga huko white house walipopata mlo wa usiku na Rais, Samia Suluhu. Yanga walifika wakiwa wamevalia nguo zao za mazoezi za Yanga walivaa jersey na sweat pants zenye logo zao. Kwa jicho letu la fashion tuliona haikukaa sawa tukauliza kwenye social media zetu na tulipata majibu tofauti tofauti, wengine wakisema hapana wangejitahidi kuvaa mavazi mazuri huku wengine wakisema walikua wanasafiri usiku huohuo kwahio walichovaa hakikua na shida.

Kwetu tunaona wangejitahidi kuvaa mavazi mazuri, hata white shirt’s na suruali nyeusi wakavaaa na moka zao nyeusi wangependeza, utajua kwamba wao ni Yanga hawaitaji kuvaa jersey kujulikana kama wao ni Yanga.

Kuhusu kusafiri wangeweza kuwa na haya mavazi kwenye bus lao wakabadilisha wakishamaliza na dinner, ili kuwa comfortable na safari tunadhani hakuna kati yao ambae angeshindwa kubadilisha mavazi mbele ya mwenzie as we all know wachezaji wa mpira wanavaaga na kubadilisha mavazi changing room pamoja.

Unaenda kukutana na Rais wa Nchi Ikulu na umevaa sweat pants? ni jambo kubwa ambalo lilikuwa linatakiwa kuwekewa uzito kidogo, kwa wanaosema walishtukizwa tunadhani hakuna mchezaji hata mmoja ambae anaweza kukosa shirt nyeupe na official trouser na viatu vizuri vya kwendea kwenye jambo zito kama hili.

Picha ya kumbukumbu ambayo imepigwa inaonekana kuwa na mambo mengi, kwa maana kila mtu kavaa chake, kuanzia viatu mpaka mavazi huyu kavaa viatu vyeupe, mwingine kavaa vyeusi, huyu ana sweat pant ina prints huyu ana nyeusi tupu, wakati wangevaa vitu vya kueleweka basi picha nayo ingekuwa na uzito kidogo.

Anyways hayo ni maoni yetu tupe ya kwako hapo chini je umeonaje kuhusu mavazi yao haya?

Related posts