SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Road to 10 Years Of Swahili Fashion Week
Habari

Road to 10 Years Of Swahili Fashion Week 

Tukiwa tunaelekea katika lile Tamasha kubwa kabisa la mitindo linalounganisha wabunifu mbalimbali kutoka Africa Mashariki na Kati Swahili Fashion Week tuna haya machache . Kwana tujue kuhusu Swahili Fashion week, Swahili Fashion Week ilianzishwa mwaka 2008 na malengo yake yalikuwa mengi yakiwepo kukuza au kuinua brand (chapa) ndogo za fashion Africa Mashariki, Kuboresha ubora na uzalishaji wa mtindo kutoka Afrika Mashariki, Kujenga fursa za bidhaa za Afrika Mashariki katika masokoya  Kimataifa tunaweza kusema kwa namna moja au nyingine Swahili Fashion Week inatoa msaada mkubwa sana kwa wabunifu, wanamitindo na wengine wengi wanao husika katika sekta ya mitindo kwa namna moja au nyingine. 

Lakini ukiangalia Swahili Fashion Week katika upande wa pili tunaweza kusema halikui, siku zote ipo palepale vitu ni vile vile kwamba tutaenda kuangalia show za mavazi siku mbili, siku ya tatu wabunifu wakubwa wata show case kazi zao halafu tuzo zitaanza kugaiwa, Swahili ina fikisha miaka 10 mwaka huu lakini kila siku unaweza kusema ni tukio linalo anza leo, maana wengine hata hatudhani kama wanalijua tamasha hili kwa kifupi hakuna mihemko.Sasa hivi ukiangalia huko mitandanioni utakutana na New York Fashion Week kila mtu jicho lake lipo huko kuona nini kinaendelea coverage yao ni kubwa tofauti na sisi ni labda bado mitindo haijakuwa kwetu au hili tamasha halipewi coverage ya kutosha. Tunadhani tujifunze kufungua milango kwa watu wengine pia hili kulinyanyua Tamasha hili.

Wasanii wajifunze kutumia hii fursa, kwa wenzetu sasa hivi unaweza kumkuta Nicki Minaj yupo kwenye NYFW, Rihanna, Ciara wote wana attend na siku karibia zote saba tofauti na kwetu ambapo wasanii wanasubiri siku ya mwisho kwenda kuangalia mavazi ya wabunifu wakubwa na kuchukua Tuzo hii inafanya zile siku mbili za kwanza zisiangaliwe sana, zinafunikwa na siku ya mwisho lakini kama wangekua wanaombwa au wana attend siku zote basi wao wanavyo ongelewa fulani yupo sehemu fulani na amevaa hivi basi hili shindano nalo lingekuwa kwa namna moja au nyingine maana watu wangekuwa curious kujua nani ana attend na atavaa nini.

Uwiano tume attend Swahili Fashion Week mara mbili mwaka juzi na mwaka jana tulicho kigundua hakuna uwiano yaani siku mbili za mwanzo wanaanza kupandishwa upcoming na ya mwisho ndio wale wenye majina makubwa tunarudi tena palepale hizi siku mbili za mwanzo zinakua hazina faida mtu anasubiri ya mwisho lakini kama ingekuwa katika siku zote tatu wanawekwa na wabunifu wakubwa wachache kushow case bidhaa zao basi ingekuwa inaongelewa kwamba siku ya kwanza kutakuwa na wabunifu wadogo fulani lakini pia wakubwa fulani na fulani wata showcase pia hii itawapa hamasa watu kutaka kwenda kuwaangalia hao wakubwa pia.

Kutumia wanamitindo wa zamani ambao wanamajina tuliiona hii mwaka juzi au mwaka jana kwa Lucky Creations ambapo alimpandisha Miriam Odemba tuikuwa impressed kwa kweli kumuona tena Miriam katika jukwaa la Swahili baada ya miaka kadhaa ya kuto kuwepo Nchini,

huko kwa wenzetu wana fanya hivyo pia kama tumeona Paris Hilton , alirudishwa mwaka huu katika runway na mbunifu Christian Cowan piaSwahili wanaweza kuwatumia watu kama Jokate Mwegelo, Hapiness Magesse, Flaviana Matata na wengine wengi waliopita tungependa kuwaoana wakirudi nyumbani na pia kuona namna gani wame improve hii haito hamsha tu hamasa za watu kuja kuattend lakini pia ma model wanao chipikia kujifunza kutoka kwao, tukifanya hivi tunaweza hata kuweka viingilio na watu wakakubali kulipa kuja kumuona fulani lakini kwa hali ya sasa tutaishia tu kualika watu bila kuingiza kipato.

Related posts

3 Comments

  1. Bassetti Kissenbezüge bestellen

    … [Trackback]

    […] Find More on that Topic: afroswagga.com/habari/road-to-10-years-of-swahili-fashion-week/ […]

  2. mounjaro study for weight loss​

    … [Trackback]

    […] Read More to that Topic: afroswagga.com/habari/road-to-10-years-of-swahili-fashion-week/ […]

  3. เด็กเอ็น

    … [Trackback]

    […] Information to that Topic: afroswagga.com/habari/road-to-10-years-of-swahili-fashion-week/ […]

Leave a Reply