Hayawi hayawi sasa yamekuwa, ile safari ya kusherekea miaka 10 ya mafanikio ya jukwaa kubwa la mitindo Afrika Mashariki na Kati imeanza rasmi.
Kwa miaka 9 maonesho ya Swahili Fashion Week yamebaki kuwa jukwaa kuu kwa Afrika Mashariki katika kuvumbua vipaji vya kipekee na mitindo maarufu ya baadae duniani. Ni ukweli usiopingika kuwa maonesho ya Swahili Fashion Week yana nia na shauku kubwa ya kuwatafuta na kuwakuza wabunifu bora wa baadae, ndio maana jukwaa la shindano la mbunifu chipukizi lijulikanalo kama Washington Benbella Emerging Designer Competition lilifikiriwa ili kutoa nafasi kwa wabunifu chipukizi na kuupeleka mbele ubunifu wao.
“Tuna furaha sana kusherekea miaka 10 ya shindano la Washington Benbella Emerging Designer Competition, tumekuwa mashaidi wa mafanikio makubwa ya washindi waliopita sababu tunashauku ya kukuza nyota wa ubunifu. Tumefarijika sana kuanza mashindano haya, katika kukamilisha miaka 10 ya uwepo wa maonesho ya mavazi “Swahili Fashion Week” tunatarajia kuona vitu vizuri Zaidi ya ubunifu wa kawaida, na Zaidi, kila kitu kiwe cha kupendeza.”.
Kila mwaka Ubora na upekee wa mitindo ya washiriki unaendelea kushangaza na kuwavutia watazamaji. Kutokana na dhamira ya maonesho ya mwaka huu ni “ Maadhimisho ya miaka 10 ya Swahili Fashion Week” hivyo basi kuna vitu vingi vya kutegemea katika maonesha haya haswa katika shindano hili la mbunifu chipukizi sababu litaonesha mitindo ya washindi wote waliopita.
“tunajitahidi kuvumbua vipaji na kuifanya kazi yao kuwa ya kimataifa, tuna wasihii wabunifu vijana kuchukua nafasi hii adimu kwa umakini na kukusanya kazi zao bora za ubunifu ambazo zitawapatia nafasi ya kuwa kati ya washiriki 10 watakaochaguliwa kuweka historia kwa kuonesha mavazi yao katika maonesho ya 10 ya Swahili Fashion Week mwezi disemba”
Kwa wabunifu chipukizi watakao vutiwa kushiriki kwenye shindano hilo watapata taarifa Zaidi kupitia fomu zetu zilizopo kwenye tovuti yetu yawww.shwahilifashionweek.com, mwisho wa kukusanya fomu hizo ni tarehe 9 Septemba mwaka huu.
Related posts
2 Comments
Leave a Reply Cancel reply
You must be logged in to post a comment.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] There you will find 45015 more Info to that Topic: afroswagga.com/habari/shindano-la-kumtafuta-mbunifu-chipukizi-linaloendeshwa-na-sfw-laanza/ […]
… [Trackback]
[…] Find More Info here on that Topic: afroswagga.com/habari/shindano-la-kumtafuta-mbunifu-chipukizi-linaloendeshwa-na-sfw-laanza/ […]