SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

SHINDANO LA MISS TANZANIA KURUDI TENA
Habari

SHINDANO LA MISS TANZANIA KURUDI TENA 

mw15tz2

Mnamo mwaka 2014 shindano la miss Tanzania lilifungiwa kutokana na mtafaruku ulio tokea mwaka huo, Mtafaruku huu ulitokea baada ya Miss alie chaguliwa ( Sitti Mtemvu)

arton2127

Sitti Mtemvu

 

kutokua na vigezo kamilifu hii ilipelekea miss huyu kujivua taji na Taji lake akapewa Miss alie mfuatia Lillian Kamazima.

lily3

Lillian Kamazima

Lakini leo tarehe 17/8/2015 ikiwa shindano hilo halija fikisha hata mwaka toka lifungiwe BASATA imetoa msamaha na kulirudisha shindano hilo. BASATA imeamua kulifungulia shindano hili baada tu ya mwandaaji wake Kampuni ya LINO International Agency Limited kufuata taratibu, kuomba radhi na kuyafanyia kazi baadhi ya mapungufu yaliyojitokeza na kutekeleza masharti aliyopewa.

Miongoni mwa  mapungufu ambayo Kampuni ya LINO imetakiwa kufanyia  kazi ni kuanza mchakato wa usajili wa mawakala – BASATA na kufanyia marekebisho kanuni na taratibu za uendeshaji wa Mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania. Aidha, LINO imewasilisha muundo wa kamati ya uendeshaji wa shindano yenye muelekeo wa kuzingatia jinsia.

Katika kuboresha na kurudisha hadhi ya shindano la Miss Tanzania, LINO International Agency Limited imepewa kibali cha muda kisichozidi miezi minne (4) kwa ajili ya maandalizi ya awali ikiwemo kukamilisha usajili wa mawakala katika ngazi zote husika.

BASATA linapenda kuwafahamisha wadau wote wa Sanaa hususan wale wa shindano la urembo la Miss Tanzania kwamba Kampuni ya LINO imetekeleza maagizo ya msingi iliyopewa kama masharti ya kufunguliwa. Na kwamba baada ya kufanyia kazi changamoto zilizokuwa zimejitokeza BASATA limeyafungulia mashindano ya Miss Tanzania kwa masharti ya kukamilisha changamoto zilizobakia.

Ni matarajio ya BASATA kwamba kampuni ya LINO itazingatia taratibu zote za uendeshaji wa matukio ya Sanaa nchini na kwamba haitarudia tena makosa yatakayopelekea kuliweka shindano hili katika hali ya kushuka hadhi na kuzua sintofahamu katika jamii

 

 

Related posts

1 Comment

  1. Study in Africa

    … [Trackback]

    […] Find More to that Topic: afroswagga.com/habari/shindano-la-miss-tanzania-kurudi-tena/ […]

Leave a Reply