SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

TAREHE RASMI YA SWAHILI FASHION WEEK YATAJWA
Habari

TAREHE RASMI YA SWAHILI FASHION WEEK YATAJWA 

 

IMG_2089

Tarehe ya jukwaa  kubwa la mtindo Afrika mashariki na kati  Swahili Fashion Week 2016 yaliyopangwa kufanyika Desemba 2016 zimetolewa. Awamu ya Tisa ya Swahili Fashion Week (SFW16) itafanyika kuanzia Desemba 02-04, katika Makumbusho ya Taifa posta  ambapo italeta pamoja  zaidi ya wabunifu 40 kutoka Afrika mashariki na kwingineko, kushuhudia kwa dhati  jukwaa hili bora la mitindo duniani.

katika Kujenga mafanikio ya  nguvu na ajabu ya misimu nane ya Swahili fashion week, jukwaa hili lina chukuliwa kuwa ni kiongozi katika  katika suala la uvumbuzi na uoneshaji wa kazi za kibunifu. mwanzilishi wa Swahili Fashion Week Mustafa Hassanali  inatarajia kujenga msingi huu kwa shauku ya hali ya juu alisema, “si  kwamba  tu tuliionyesha  dunia kuwa kina cha vipaji vya ubunifu nchini Tanzania na Afrika ni vya ajabu kweli, lakini sasa tuna vyombo vya habari kutoka nchi mbalimbali wanasubiri kuhudhuria na kuunga mkono jukwaa hili na kulikuza  duniani kote. Kama mithali hii ya Afrika inavyosema “ kama unataka kwenda haraka nenda mwenyewe, kama unataka kwenda mbali nenda pamoja”

Mustafa aliongeza kuwa  , “lengo la kuendeleza mtindo ya kiafrika  bado lipo katika mstari wa mbele katika yale ambayo tumelenga kuyafanya, na kupitia kutanuka kwa jukwaa hili kutokana na   vyombo mbali mbali vya habari, katika Tanzania, Afrika na kwengineko  kwa ujumla zinaona kwamba kuna njia mbadala kwa bidhaa zetu kutoka nje, Tuna nia ya kukuza thamani ya bidhaa, kupigania dhana ya bidhaa zinazotangenezwa afrika na kujenga bidhaa zenye mizizi ya afrika ”

toleo la tisa ya Swahili Fashion Week itaendelea kuwa kivutio  katika maonesho yote ya wiki nchini afrika  pamoja na wabunifu wa ndani, kikanda na kimataifa wakinyesha hisia zao za dhati. Mwaka huu tutakuwa na wabunifu 18 wa Kitanzania na 12 wabunifu wa kimataifa kuonyesha Jijini Dar es Salaam.

“tunaendelea kuwaomba jamii kukuza Tasnia ya  ubunifu na kuvaa fahari ya vilivyo tengenezwa  za Afrika hasa dhana ya Kitanzania. Vipaji vya ndani vinahitaji kulelewa na kuvihusisha bidhaa zinazotambulika ulimwenguni, kutoa ni moyo si utajiri, hivyo tunatazama mbele katika kuanza  kuwasaidia kampuni ndogo ndogo na mashirika hili kuwezesha biashara hii ya mitindo ya ubunifu.” Lightness Kitua  mratibu Swahili Fashion Week

Katika tukio hili la mwaka huu, mbali na maonyesho vya mavazi jukwaani unafanyika kila jioni kwa kipindi cha siku tatu kutoka 08:30 na kuendelea, na wakati mchana  kutakuwa na tamasha  la ununuzi wa bidhaa ambapo waonyeshaji mbalimbali watakuwa wakionyesha na kuuza kazi mbalimbali za  mikono , sanaa na vifaa. Katika siku ya mwisho  ya Desemba 4, maonesho yatasherekea maadhimisho  ya sekta ya mitindo nchini kwa kutoa tuzo 24 kwa awshindi wataotangazwa usiku huu kupitia vipengele mbalimbali.

Swahili Fashion Week na tuzo 2016 ina ahidi   kushinikiza teknolojia na kuonyesha uzalishaji wa juu na wa mwisho kabisa katika  siku tatu za mtindo, uzuri, na mtindo wa maisha ya onesho hili na utembeaji wa kimataifa kutoka kwa wanamitindo na kuonyesha tamaduni mbali mbali zisizo sahaulika  ambazo zinaendelea  kuiweka Tanzania uangalizi wa kimataifa.

Swahili Fashion Week 2016 na Tuzo limeandaliwa na 361 degrees, kudhaminiwa na EATV, East Africa Radio, Darling Hair, Colosseum Hotel & Spa, Tanzania Printers Ltd,  Majira , Busines Times, Fabcars, Darlife, Asila’s Make up, Nexia Sj, Green telecom, A1outdoor, Epidor, Eventlites, Jumia Market, Michuz Blog , BASATA (Baraza La Sanaa La Taifa),

Fomu za Kupata kibali kwa waandishi wa habari, tafadhari sajili katika votuti yao www.swahilifashionweek.com

Related posts