SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Vuta Ni Kuvute Ya Uwakilishi Miss World 2021
Habari

Vuta Ni Kuvute Ya Uwakilishi Miss World 2021 

Bado vuguvugu la nani ataenda kuiwakilisha Nchi katika mashindano ya Miss World 2021 linaendelea, Ikumbukwe week iliyopita Miss Tanzania Organization walitoa Tamko la kumuengua Rosey Manfere kuwakilisha Nchi katika Miss World badala yake aende Miss number 2 Juliana Rugumisa. Basata iliwaita pande zote mbili na kutoa Tamko la kwamba Rose anastahili kuwakilisha Taifa katika mashindano hayo.

Well Miss Tanzania Organization imeonekana kushikiria msimamo wake na kusema kama haki haitopatikana BASATA basi itapatikana hata mahakani na pia wameendelea kumshtumu Rose kwa kuwa mdanganyifu.

ELIMU KWA WADAU WETU inaendelea..🇹🇿👑

Mungu hadhihakiwi. Hata Yesu Kristu alisulibiwa msalabani na dunia nzima kumgeuka ila watu wema walikua nae na Mungu mwenyezi na ushindi ukawa kwake.

Kwahiyo kwa sababu Pilato alisema asulubiwe basi mamlaka ilikua sahihi? Wote mmaujua ukweli. Hivi watu makini hawajiulizi .Mbona mshindi wa kwanza alishinda, pili The Look ilishawekeza Kwake , sasa kama hasara ni ya nani? Iweje waanze upya kuwekeza kwa mtu mwingine?.

Ni kwa sababu tunajukumu kubwa la kumpeleka mtu anaewakilisha TANZANIA nzima. Dhambi ya kumpeleka mtu aliyeonyesha KUKOSA sifa ya uwakilishi wa nchi na lana yake tutaibeba sisi ( ilihali tulizigundua kasoro mapema) ndio maana Sheria na kanuni ziliwekwa ikitokea tatizo kubwa kama hilo kamati inapaswa kuchukua hatua gani? Tumetekeleza . kamati imeenda mbele kupunguza makali ya adhabu kama kuweka ‘pending’ swala la kumvua kabisa taji na kumnyanganya zawadi ili kumpa nafasi ya kujitafakari na kujifunza. Na ikishindikana ndio ikamilishe adhabu hiyo.

Tunatimiza wajibu wetu kikamilifu 🙏 Sisi tunasonga mbele na watanzania makini !!
Kazi zinaendelea.

NO ONE IS ABOVE THE LAW

BASATA wasimamie misingi ya SHERIA na KANUNI
watakua salama. Haki isipopatikana BASATA itapatikana MAHAKAMANI

With Tanzania representative @juliana_rugumisa usikose kumfuatilia leo akiendelea na majukumu yake ya ‘Beauty with a purpose’ Huyu binti anatushangaza na uchapaji kazi wake. Tunamuombea na anaenda kuishangaza dunia @juliana_rugumisa THE NEW FACE OF AFRICA FROM TANZANIA TO THE WORLD 🇹🇿”.

Huku wakiihutumu BASATA kwa kumkingia kifua Rose Manfere.

Tunahitaji kujua kama BASATA ya mwaka mmoja nyuma ni BASATA Ile ile ya sasa??

Sababu za msingi kwa BASATA ni zipi???

Sababu za msingi ni zile zilizopo kwenye kanuni na sheria sio zinazosomwa na utashi wa mtu aliyeshika kiti. Zingekua sio za msingi zisingekuwepo kwenye kanuni ya sheria.

Sisi ni wawekezaji katika sanaa tunawekeza pesa na rasilimali na tunatii na kufuata sheria na kanuni hatutakubali kuonewa.

Tumeshirikishana kila hatua ghafla mmetugeuka.

NO ONE IS ABOVE THE LAW

At this point its getting ghetto, well #afromates Thoughts?

Related posts

2 Comments

  1. pg slot

    … [Trackback]

    […] Here you will find 89028 additional Information on that Topic: afroswagga.com/habari/vuta-ni-kuvute-ya-uwakilishi-miss-world-2021/ […]

  2. บ้านมือสอง

    … [Trackback]

    […] Read More Info here to that Topic: afroswagga.com/habari/vuta-ni-kuvute-ya-uwakilishi-miss-world-2021/ […]

Comments are closed.