Mlimbwende Zawadi Dotto ameibuka kidedea katika Mashindano ya Miss Albinism Kanda ya Ziwa yaliyofanyika usiku wa Kuamkia leo Jijini Mwanza.
Miss Zawadi mwenye umri wa miaka 17 (mwanafunzi) ameibuka mshindi katika Mashindano hayo ambayo ni maalumu kwa ajili ya Watu wenye ulemavu wa ngozi kwa ajili kuonyesha umahiri wao katika tasnia ya ulimbwende hii ikiwa pia ni ishara ya kwamba watu wenye ulemavu wa ngozi wanaweza kushiriki katika shughuli na mashindano mbalimbali.
Katikati ni Mshindi wa Kwanza, Kulia Mshindi wa Pili na Kushoto Mshindi wa Tatu.
Mashindano hayo yanaandaliwa na Taasisi ya kusaidia Watu wanaoishi katika Mazingira hatarishi iitwayo SAVE VULNERABLE FOUNDATION ya Jijini Dar es Salaam.
Washiriki Saba wa Miss Albinism 2016 Kanda ya Ziwa na umri wao katika mabano ambapo kutoka Kushoto ni Hajra Sadru (22), Antonia Mathias William (17), Furaha Edward John (17), Pendo Faustine (15), Zabibu Abdallah (18), Zawadi Dotto (17) pamoja na Asteria Christopher.
Mratibu wa Shirika hilo Alexander Exaud Mutowo ametanabaisha kwamba, baada ya mashindano hayo kukamilika kwa kanda zote nchini, Washindi wa Kanda hizo watashindanishwa Jijini Dar es salaam ili kumpata Mshindi wa Kitaifa wa MISS ALBINISM 2016.
Related posts
4 Comments
Leave a Reply Cancel reply
You must be logged in to post a comment.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Find More to that Topic: afroswagga.com/habari/zawadi-dotto-miss-albinism-kanda-ya-ziwa-2016/ […]
… [Trackback]
[…] Read More on that Topic: afroswagga.com/habari/zawadi-dotto-miss-albinism-kanda-ya-ziwa-2016/ […]
… [Trackback]
[…] Find More Information here to that Topic: afroswagga.com/habari/zawadi-dotto-miss-albinism-kanda-ya-ziwa-2016/ […]
… [Trackback]
[…] Information to that Topic: afroswagga.com/habari/zawadi-dotto-miss-albinism-kanda-ya-ziwa-2016/ […]