Je? Ndo umeanza safari yako ya kukuza nywele na nywele zako hazikui haraka kama ulivyotegemea? Basi inawezekana hautunzi nywele zako vizuri. Nitakuelezea njia unazoweza kutumia kukuza nywele zako haraka na kukujulisha makosa gani unayafanya yanyositisha ukuaji wa nywele zako.
MAKOSA YA SABABISHAYO NYWELE ZAKO KUTOKUKUA HARAKA;
- Kosa la kwanza, watu wengi wana blow dry au wananyoosha nywele zao mara kwa mara. Mtu akifanya hivi basi, ataziua nywele zake na zitaanza kukatika wakati wa kuchana au mda wowote. Basi inabidi upunguze kutumia vifaa kama hivi ili nywele zako zikue ( Hata kama umepaka dawa).
- Pili, tunavyoziachia nywele na kuzistyle kusuka rasta, nywele za kawaida au kushonea weaving zinakubalika, ila ukizichana na kuzisbana nywele basi hapo inaweza kuziharibu au kuzikata nywele.
- Pia, kutokukata ncha baada ya mda, ncha zinaweza kuanza kuchanika na inabidi uzikate ili nywele zikue vizuri kwasababu ncha huchangia kwenye kusitisha ukuaji wa nywele na kukata nywele. Unaweza kukata incha1-2 au cm 2-2.5 baada ya miezi mitatu au minne.
MBINU ZA KUKUZA NYWELE HARAKA;
- Kwanza, inabidi uzisuke nywele zako mara kwa mara ilizisiharibike au zisikatike. Hivi utaweza hata kuzuia ncha zilizoharibika. Kama hujisikii kusuka nywele au kushonea weaving basi unaweza kuzibana kwa juu au kuzifunga na kitambaa ila ni lazima kitambaa kiwe cha silk ili nywele zako zisiharibike ( unaweza kukitumia hata wakati wa kulala).
- Pili, inabidi upake mafuta kwenye kichwa chako mara kwa mara, sana sana unapojisikia kama kichwa kimekauka au kama kinawasha. Mafuta mazuri kutumia kwaaji ya ukuaji wa nywele ni mafuta ya nazi, castor, Moroccan, Jamaican au lavender. Ila hata mafuta mengine yeyote unayotumia ilayasiwe ya mgando.
- Pia, usizioshe nywele na shampu mara kwa mara kwasababu shampoo inaondoa mafuta kwenye kichwa na nywele zako. Basi, inabidi uoshe nywele na conditioner kama unaona nywele zako sio chafu sana, ila kama unaonanywele zako ni chafu basi osha na shampu. Itakuwa bora ukipaka mafuta kabla ujaosha nywele na shampu na uoshe nywele zako kila baada ya wiki moja na kama zinakatika basi, osha baada ya wiki mbili au tatu.
- Kula vyakula vingi vyenye protini kama kuku, mtindi, maharagwe au nyama yoyote.
Related posts
5 Comments
Leave a Reply Cancel reply
You must be logged in to post a comment.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Read More on on that Topic: afroswagga.com/hair/fanya-haya-ukuze-nywele-zako-haraka/ […]
… [Trackback]
[…] Find More Information here on that Topic: afroswagga.com/hair/fanya-haya-ukuze-nywele-zako-haraka/ […]
… [Trackback]
[…] Find More Information here on that Topic: afroswagga.com/hair/fanya-haya-ukuze-nywele-zako-haraka/ […]
… [Trackback]
[…] Read More Information here on that Topic: afroswagga.com/hair/fanya-haya-ukuze-nywele-zako-haraka/ […]
… [Trackback]
[…] Find More here on that Topic: afroswagga.com/hair/fanya-haya-ukuze-nywele-zako-haraka/ […]